WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, December 9, 2024

TIMU ZA TANZANIA ZANG'ARA MASHINDANO YA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YANAYOENDELEA MOMBASA NCHINI KENYA

Wachezaji za Bunge la Tanzania wakishangilia ushindi walioupata katika michezo mbalimbali katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Nchini Kenya. 

 

Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Kamba Wanaume wakivuta kamba dhidi ya wapinzani wao Timu ya Kenya katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Nchini Kenya.Timu ya Bunge la Tanzania iliibuka kidedea katika mchezo huo.

Wachezaji za Bunge la Tanzania wakiongozwa na Mheshimiwa Salma Kikwete wakishangilia ushindi wa riadha katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Nchini Kenya
Wachezaji za Bunge la Tanzania wakiongozwa na Mheshimiwa Salma Kikwete wakishangilia ushindi wa riadha katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Nchini Kenya

Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Kamba Wanawake wakivuta kamba dhidi ya wapinzani wao Timu ya Kenya katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Nchini Kenya.Timu ya Bunge la Tanzania iliibuka kidedea katika mchezo huo

Mchezaji wa Timu ya Riadha kutoka Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Anatropia Theonist akishiriki katika mbio za mita 1500 katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Nchini Kenya. Mheshimiwa Anatropia alishika nafasi ya kwanza katika mbio hizo na mbio za mita 400

Timu ya Bunge ya Mpira wa Wavu Wanawake wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mchezo kati yao na Timu ya Bunge ya Sudan ya Kusini kushindwa kufanyika kutokana na timu hiyo kutofika uwanjani. Timu za Bunge la Tanzania zipo Mombasa Nchini Kenya kushiriki michezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki

 

Sunday, December 8, 2024

TIMU NNE ZA BUNGE LA TANZANIA LEO ZIMECHUANA NA TIMU MBALIMBALI KATIKA MASHINDANO YA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YANAYOENDELEA MOMBASA KENYA

 

Mfungaji wa bao la pekee wa mchezo katika ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge la Tanzania Mheshimiwa Simai Hassan Sadiki akichauna vikali na mpinzani wake wakati timu hiyo ilipochuana na Timu ya Mpira wa Burundi katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Kenya. Mchezo huo ulimalizika kwa suluhu ya mabao 1-1

Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Kikapu Wanaume wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo kati yao na Timu ya Bunge la Sudan ya Kusini, hata hivyo Timu ya Bunge la Tanzania ilipewa alama kutokana na mpinzani wao kushindwa kufika uwanjani. Timu za Bunge za Tanzania zinaendelea na mashindano ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya
Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Kikapu Wanawake wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo kati yao na Timu ya Bunge la Sudan ya Kusini, hata hivyo Timu ya Bunge la Tanzania ilipewa alama kutokana na mpinzani wao kushindwa kufika uwanjani. Timu za Bunge za Tanzania zinaendelea na mashindano ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya.

Mchezaji wa Mpira wa pete kutoka Timu ya Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Esther Matiko akijiandaa kufunga wakati timu hiyo ilipochuana na Timu ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) katika mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mchezo huo ulifanyika katika Uwanja wa Aghakani Jijini Mombasa, Kenya na ulimalizika kwa Timu ya Tanzania kuifunga EALA mabao 50-0

Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge la Tanzania ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya Timu ya Bunge ya Burundi katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Kenya. Mchezo huo ulimalizika kwa suluhu ya mabao 1-1

 

Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Pete wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mheshimiwa Joseph Ntakirutimana kabla ya kuanza kwa mchezo na Timu ya Bunge la EALA. Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Aghakani Jijini Mombasa, Kenya, ulimalizika kwa Timu ya Tanzania kuifunga Timu ya EALA mabao 50-2.

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mheshimiwa Joseph Ntakirutimana akisalimiana na Mchezaji wa Timu ya Mpira wa Pete kutoka Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Bupe Mwakang’ata wakati timu hiyo ikijiaanda kuingia uwanjani kuchuana na Timu ya EALA. Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Aghakani Jijini Mombasa, Kenya, ulimalizika kwa Timu ya Tanzania kuifunga Timu ya EALA mabao 50-2.

Saturday, December 7, 2024

PICHA ZA UFUNGUZI WA MASHINDANO YA MICHEZO YA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI, MOMBASA KENYA

Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika matembezi kuelekea Uwanja wa Likoni kwa ajili ya hafla ya ufunguzi wa wa Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya. Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto amefungua rasmi mashindano hayo yalioanza tarehe 6 Desemba, 2024 na yanatarajiwa kumalizika Desemba 17, 2024

Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mheshimiwa Abbas Tarimba akizungumza katika ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya. Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto amefungua rasmi mashindano hayo yalioanza tarehe 6 Desemba, 2024 na yanatarajiwa kumalizika Desemba 17, 2024.



 Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya 6-17 Desemba, 2024 huku Timu ya Bunge ikiwa inashiriki michezpo mbalimbali

Waheshimiwa Wabunge ambao ni wanamichezo wa timu mbalimbali za Bunge wakiwa katika hafla ya ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya. Rais wa Kenya Mheshimiwa William Ruto amefungua rasmi mashindano hayo yalioanza tarehe 6 Desemba, 2024 na yanatarajiwa kumalizika Desemba 17, 2024