Mfungaji wa bao la pekee wa mchezo katika ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge la Tanzania Mheshimiwa Simai Hassan Sadiki akichauna vikali na mpinzani wake wakati timu hiyo ilipochuana na Timu ya Mpira wa Burundi katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Kenya. Mchezo huo ulimalizika kwa suluhu ya mabao 1-1
Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Kikapu Wanawake wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo kati yao na Timu ya Bunge la Sudan ya Kusini, hata hivyo Timu ya Bunge la Tanzania ilipewa alama kutokana na mpinzani wao kushindwa kufika uwanjani. Timu za Bunge za Tanzania zinaendelea na mashindano ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika Mombasa Nchini Kenya.

Mchezaji wa Mpira wa pete kutoka Timu ya Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Esther Matiko akijiandaa kufunga wakati timu hiyo ilipochuana na Timu ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) katika mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mchezo huo ulifanyika katika Uwanja wa Aghakani Jijini Mombasa, Kenya na ulimalizika kwa Timu ya Tanzania kuifunga EALA mabao 50-0
Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge la Tanzania ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya Timu ya Bunge ya Burundi katika mashindano ya Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mombasa Kenya. Mchezo huo ulimalizika kwa suluhu ya mabao 1-1

Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Pete wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mheshimiwa Joseph Ntakirutimana kabla ya kuanza kwa mchezo na Timu ya Bunge la EALA. Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Aghakani Jijini Mombasa, Kenya, ulimalizika kwa Timu ya Tanzania kuifunga Timu ya EALA mabao 50-2.
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mheshimiwa Joseph Ntakirutimana akisalimiana na Mchezaji wa Timu ya Mpira wa Pete kutoka Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Bupe Mwakang’ata wakati timu hiyo ikijiaanda kuingia uwanjani kuchuana na Timu ya EALA. Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Aghakani Jijini Mombasa, Kenya, ulimalizika kwa Timu ya Tanzania kuifunga Timu ya EALA mabao 50-2.
No comments:
Post a Comment