WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, August 23, 2018

KAMATI ZA BUNGE ZAENDELEA KUKUTANA JIJINI DODOMA

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (P.I.C) wakiendelea na Kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika leo Jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (P.I.C) Mheshimiwa Dkt. Raphael Chegeni akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa  Kamati hiyo iliyokutana leo Jijini Dodoma.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (P.I.C) Mheshimiwa Esther Mmasi akichangia jambo katika  Kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika leo Jijini Dodoma.

Tuesday, August 21, 2018

WITO WA WADAU KUTOA MAONI KUHUSU MISWADA MITANO YA SHERIA



SPIKA WA BUNGE MHE NDUGAI AHUDHURIA SEMINA YA UMATI

Mheshimiwa Spika Job Ndugai akipata picha ya pamoja na waheshimiwa wabunge na watendaji wengine waliohudhuria semina ya afya ya uzazi katika hoteli ya morena leo jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisikiliza kwa makini mmoja wa watoa mada ya kuhusu afya bora ya uzazi katika semina iliyoandaliwa kwa ajili ya wabunge iliyofanyika leo katika hoteli ya morena jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai ahudhuria semina inayohusu afya ya uzazi na malezi bora iliyoandaliwa na Chama cha UMATI kushirikiana na Chama cha kutokomeza rushwa APNAC iliyofanyika leo Mjini Dodoma Tanzania.


Saturday, August 18, 2018

MHE. SPIKA AMJULIA HALI WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHUMBILI ALIKOLAZWA KWA AJILI YA MATIBABU


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangalla baada ya kumtembelea kwa lengo la kumjulia katika Hospitali ya Taifa ya Mhumbili alikolazwa kw ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangalla baada ya kumtembelea kwa lengo la kumjulia hali katika Hospitali ya Taifa ya Mhumbili alikolazwa kw ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari, pembeni ni Katibu wa Bunge, Ndugu. Stephen Kagaigai

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwa ameambatana na Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai na baadhi wa Waheshimiwa Wabunge wamemtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangalla kwa lengo la kumjulia hali katika Hospitali ya Taifa ya Muhumbili alikolazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari.