WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, November 27, 2020

SPIKA NDUGAI MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI YA 46 YA CHUO CHA IFM

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiwa ameambatana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta wakiwasili katika Mahafali ya 46 chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai  akizungumza na Wahitimu wa Chuo cha  Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakati wa  Mahafali ya 46 chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai  akizungumza na Wahitimu wa Chuo cha  Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakati wa  Mahafali ya 46 chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

1.    Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai  (wa pili kushoto) akimpatia zawadi Mwanafunzi Bora kwa Wahitimu wa kozi zote za Shahada wa  Chuo cha Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Bw. Robin Micky Goliama wakati wa  Mahafali ya 46 chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka  kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Tadeo Satta, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Prof. Emmanuel Mjema na Mwakilishi wa Waziri wa Fedha ambaye pia Naibu Mkurugenzi wa Mipango katika Wizara ya Fedha, Bw. David Mwankenja.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai  (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Menejimenti  na Wanafunzi Bora katika kozi mbalimbali wa   Chuo cha Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakati wa  Mahafali ya 46 chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na  Mkuu wa Chuo cha  Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Prof. Tadeo Satta (kulia) na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Prof. Emmanuel Mjema (kushoto) wakati wa  Mahafali ya 46 chuo hicho yaliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.


 

OFISI YA BUNGE YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZA BUNGE

Waandishi wa habari za Bunge wakifuatilia kwa makini mada zilizowasilishwa kwenye Mafunzo ya Waandishi hao yaliyofanyika kwenye hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. 
Mwandishi wa habari za Bunge kutoka gazeti la Mwananchi, Ndg. Sharon Sauwa akiuliza shwari kwa Mtoa Mada (hayuko pichani) kwenye Mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. 
Mwandishi wa habari za Bunge kutoka gazeti la Uhuru, Ndg. Mussa Yusuph akiuliza shwari kwa Mtoa Mada (hayuko pichani) kwenye Mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. 
Mwandishi wa habari za Bunge kutoka Star TV, Ndg. Mozes Blaya akichangia jambo kwenye Mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. 
Mwandishi wa habari za Bunge kutoka Global TV, Ndg. Mohamed Zengwa akichangia jambo kwenye Mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. 


Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali  Dkt.Hassan Abbasi akiwasilisha mada juu ya ‘Mambo Muhimu ya Kuzingatiwa na Waandishi wa Habari za Bunge’ kwenye mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma









Tuesday, November 24, 2020

SPIKA NDUGAI AWAAPISHA WABUNGE 19 WA VITI MAALUM WA CHADEMA JIJINI DODOMA

Wabunge Wateule wa Viti Maalum kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA wakisubiri kula kiapo kwenye viwanja vya Bunge Jijini Dodoma 

SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Halima Mdee kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Esther Matiko kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Esther Bulaya kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Cecilia Pareso kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Halima Mdee akiongea jambo kwa niaba ya Wabunge wengine wa CHADEMA walioapishwa katika  Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. 

SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai na Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai katika picha ya pamoja na Wabunge wa Viti Maalum CHADEMA mara baada ya kuwaapisha. 


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai amewaapisha wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha, Spika wa Bunge alieleza utaratibu wa kikatiba uliotumika kuwapata wabunge hao pamoja na utaratibu wa kikanuni wa kuwaapisha katika kipindi ambacho hakuna Mkutano wa Bunge.

Aidha, aliwaahidi wabunge hao kuwalinda na kuwapa ushirikiano wa kila namna licha ya uchache wao Bungeni.

“Nawapongeza sana na mimi kama Spika jukumu langu ni kuwalinda walio wachache, hivyo naahidi kuwalinda na kuwapa ushirikiano wa kila hali wakati wa kutekeleza majukumu yenu,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge wenzake, Mheshimiwa Halima Mdee alimshukuru Spika kwa kuwapokea na kuahidi kufanya kazi kwa bidii kuwatumikia Watanzania.

Waheshimiwa Wabunge waliokula kiapo ni Halima Mdee, Grace Tendega, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Esther Bulaya, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.

 

Wengine ni Agnesta Kaiza, Nusrat Hanje, Asia Mohamed, Felister Njau na Stela Fiyao.

 

---------