




SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai na Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai katika picha ya pamoja na Wabunge wa Viti Maalum CHADEMA mara baada ya kuwaapisha.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai amewaapisha wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kuwaapisha, Spika wa Bunge alieleza utaratibu wa kikatiba uliotumika kuwapata wabunge hao pamoja na utaratibu wa kikanuni wa kuwaapisha katika kipindi ambacho hakuna Mkutano wa Bunge.
Aidha, aliwaahidi wabunge hao kuwalinda na kuwapa ushirikiano wa kila namna licha ya uchache wao Bungeni.
“Nawapongeza sana na mimi kama Spika jukumu langu ni kuwalinda walio wachache, hivyo naahidi kuwalinda na kuwapa ushirikiano wa kila hali wakati wa kutekeleza majukumu yenu,” alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wabunge wenzake, Mheshimiwa Halima Mdee alimshukuru Spika kwa kuwapokea na kuahidi kufanya kazi kwa bidii kuwatumikia Watanzania.
Waheshimiwa Wabunge waliokula kiapo ni Halima Mdee, Grace Tendega, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Esther Bulaya, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.
Wengine ni Agnesta Kaiza, Nusrat Hanje, Asia Mohamed, Felister Njau na Stela Fiyao.
---------
No comments:
Post a Comment