WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, April 15, 2024

SPIKA DKT. TULIA MGENI RASMI BUNGE MARATHON















SPIKA DKT. TULIA MGENI RASMI BUNGE MARATHON

·         Ashiriki katika mbio za km 5

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), mgeni rasmi katika mbio za Bunge Marathon zilizofanyika tarehe 13 Aprili, 2024 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mbio hizo za Bunge marathon zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ndg. Kaspar Mmuya, Waheshimiwa Wabunge na Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc.

Lengo likiwa ni kuchangisha kiasi cha Shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Bunge.

Huku kauli mbiu ikiwa ni “Shiriki Michezo kwa Maendeleo ya Taifa Letu”.

Tuesday, March 26, 2024

KAMATI YA LAAC IMEIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASWA MKAONI SIMIYU KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MRADI WA JENGO LA DHARULA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA HIYO NA UJENZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA CHAKI


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wakiangalia vifaa vya matibabu katika Jengo la Dharula la Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Moan Simiyu wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua jengo hilo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wakionyeshwa mojawapo ya mtambo wa kutengeneza chaki wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua  Mradi wa Kiwanda cha kutengeneza Chaki na Vifungashio cha Ng’ami kilichopo Halmashauri ya Maswa Mkoani Simiyu.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),Mheshimiwa Stansalaus Mabula akizungumza na watendaji wa Kiwanda cha Kutengeneza Chaki na Vifungashio cha Ng’ami wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Kiwanda hicho kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.

 

 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa katika chumba cha kuhifadhi mitungi ya oksijeni katika Jengo la Dharula la Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua jengo hilo.

 

Sunday, March 24, 2024

KAMATI YA LAAC IMEKAGUA MRADI WA SHULE YA SEKONDARI NA ZAHANATI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA

 

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakikagua mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Kata ya Kigera katika Manispaa ya Musoma Mkoani Mara wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi huo.

 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), Mheshimiwa Stansalus Mabula akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mkoani Mara wakati Kamati hiyo ilipotembelea na mradi wa ujenzi wa Zahati ya Rwamlimi katika Manispaa hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), Mheshimiwa Stanslaus Mabula akizungumza wakati Kamati ya LAAC ilipomtembelea Mkuu wa Mkoa Ofisini kwake katika Manispaa ya Musoma, kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Said Mtanda na kushoto ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mheshimiwa Patrick Gumbo.

Saturday, March 23, 2024

KAMATI YA BUNGE YA LAAC IMETEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI MKOANI MARA

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiwa na wajumbe wa Kamati hiyo wakikagua ujenzi wa msingi katika moja ya wodi ya Hospitali ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Marawakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali hiyo.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakikagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi huo
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), Mheshimiwa Stansalus Mabula akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali hiyo.