Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job
Ndugai akiwahutubia Wabunge waliohudhuria Mkutano wa Wabunge wa Mabunge ya
Afrika Mashariki (EALA) leo Jijini Dar es Salaam.
|
Baadhi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA)
wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali wakati wa Mkutano wa Wabunge wa
Mabunge ya Afrika Mashariki (EALA) leo Jijini Dar es Salaam.
|
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
amefungua semina ya Wabunge wa Mabunge ya Afrika Mashariki (Inter-Parliamentary
Relation Seminar -Nanyuki IX) inayofanyika Jijini Dar es saalm
kuanzia tarehe 2 hadi 4 Machi 2016 na kuwataka wabunge hao kuangalia kwa undani
sheria zinazosimamia uchaguzi katika nchi za Afrika Mashariki ili kuondoa
kasoro zinazojitokeza mara kwa mara.
Mhe. Samia amesema chaguzi nyingi zimekuwa
na kasoro katika nchi za Afrika Mashariki hivyo mapendekezo yatakayopatikana
katika mkutano huo yatasaidia kuwa na chaguzi huru na zinazofuata demokrasia
katika mataifa ya Afrika Mashariki.
Kuhusu Uchaguzi wa Zanzibar Mhe. Samia
amewahakikishia Wabunge hao kuwa hakutakuwa na vurugu na kwamba uchaguzi
utakuwa huru na haki na kuwasihi Wazanzibari kuwa watulivu na kujitokeza kwa
wingi kupiga kura.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Tanzania
Mhe. Job Ndugai amesema amefurahi kuona mkutano huo umechagua suala la uchaguzi
kuwa Dhima kuu ya mkutano na kwamba anaamini kupitia mkutano huo
kutapatikana mawazo mapya kwenye masuala ya demokrasia, utawala wa sheria, na
uchaguzi.
Awali akimkaribisha Makamu wa Rais, Spika wa
Bunge la Tanzania Mhe. Ndugai amesema huu ni wakati mzuri kujadili masuala ya
uchaguzi kwa sababu baadhi ya nchi wanachama wametoka katika uchaguzi na
kuwaomba wabunge hao kujadili kwa kina suala la uchaguzi na utamaduni wa
kuachiana madaraka kwa amani ili kuepuka vurugu.
Naye Spika wa Bunge la Afrika Mashariki
(EALA) Mhe. Daniel Kidega amesema mkutano huo utaangalia namna ya kuboresha
demokrasia katika nchi wanachama na kuangalia jinsi Mataifa ya Afrika Mashariki
yanavyofuata sheria za kimataifa zinazohusu masuala ya uchaguzi.
Mhe. Kidega pia amewatakia wazanzibari
uchaguzi mwema unaotarajia kufanyika hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment