WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, April 29, 2016

SPIKA WA BUNGE AKABIDHI UENYEKITI WA JUKWAA LA MASPIKA WA NCHI WANACHAMA WAJUMIYA YA AFRIKA MASHARIKI


Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimkabidhi Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega baada ya Tanzania kumaliza muda wake. Kulia ni Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimpisha Spika wa Bunge la Afrika mashariki kuongoza kikao mara baada ya kumkabidhi UenyekitiSpika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Bunge la Seniti la Burundi Mhe Reverien Ndikuriyo wakati wa Mkutano wa Mkutano wa kumi na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha.


Spika wa Bunge Job Ndugai akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mhe Jeanne Uwimanimpaye wakati wa Mkutano huo.


           Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai  (wa kwanza kulia) akifurahia jambo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega  (katikati) na Spika wa Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi wakati wa Mkutano wa Mkutano wa kumi na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha.

Maspika na Manaibu Spika wa Mabunge na Maseneti ya nchi za Jumuiya za Afrika Mashariki katika picha ya pamoja baada ya Mkutano wa kumi na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Maspika na Manaibu Spika wa Mabunge na Maseneti ya nchi za Jumuiya za Afrika Mashariki (waliokaa) pamoja na Makatibu wa Mabunge hayo (waliosimama) katika picha ya pamoja baada ya Mkutano wa kumi na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiongoza kikao cha Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kukabidhi Uenyekiti wa Jukwaa hilo baada ya muda wa Tanzania kumalizika. Kulia ni Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah.

No comments:

Post a Comment