WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, May 2, 2016

WAGENI WALIOTEMBELEA BUNGE LEO MEI 2,2016.

Mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement akiwa Bungeni leo mjini Dodoma Mwanafunzi huyo alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani.

 Mashududa walihusika katika zoezi la kuchanganya udongo wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964, wakiwa Bungeni leo mjini Dodoma kwa  mwaliko wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango wao katika kuuenzi na kuulinda Muungano wa Tanzania.

Mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement (wa pili kushoto) ambaye alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani akiwa na wanafunzi wenzake Bungeni leo mjini Dodoma.

Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na mashuhuda waliohusika katika zoezi la kuchanganya udogo wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964. Mashuhuda hao walikuja kutembelea Bunge leo Mei 2, 2016.

Naibu Spika Dkt Tulia Ackson na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe January Makamba wakiwa katika picha ya pamoja na mashuhuda waliohusika katika zoezi la kuchanganya udogo wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964. Mashuhuda hao walikuja kutembelea Bunge leo Mei 2, 2016.

No comments:

Post a Comment