Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) amefanya mabadiliko
mengine ya baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge ili kuzingatia maombi
ya baadhi ya Wabunge pamoja na mahitaji mapya yaliyojitokeza wakati wa
utekelezaji wa shughuli za Kamati za Bunge.
Kwa mujibu wa taarifa yake, mabadiliko hayo yamefanywa kwa
mujibu wa Kanuni ya 116(3) na (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili
2016 ambapo yamehusisha maeneo manne ikiwemo; Kuhamishwa kwa baadhi ya wajumbe
wa Kamati, Kualikwa kwa baadhi ya wajumbe katika Kamati ya Bajeti, Baadhi ya
Wajumbe wa kamati ya Haki, Maadili, na Madaraka ya Bunge kuondolewa pamoja na Uteuzi
wa wajumbe wapya katika kamati ya Haki, Maadili, na Madaraka ya Bunge.
Mabadiliko hayo ya wajumbe kwenye kamati yanaanza mara moja
ambapo orodha ya wajumbe waliobadilishwa kamati na nafasi zao ni kama
ifuatavyo; Wajumbe wanaohamishwa Kamati ni pamoja na Mhe. Ezekiel Magoyo Maige,
(Mb) ambaye alikuwa katika Kamati ya Nishati na Madini na kwa sasa anahamia
Kamati ya PAC, Mhe. Allan Joseph Kiula (Mb) ambaye alikuwa katika Kamati ya Mambo
ya Nje, Ulinzi na Usalama na kwa sasa anahamia Kamati ya PAC, Mhe. Omary
Tebweta Mgumba (Mb) ambaye alikuwa katika Kamati ya Sheria Ndigi na kwa sasa
anahamia Kamati ya PAC, Mhe. Rhoda Rdward Kunchela (Mb) ambaye alikuwa katika
Kamati ya Masuala ya UKIMWI na kwa sasa anahamia Kamati ya PAC.
Wengine ni Mhe. Joseph George Kakunda (Mb) ambaye alikuwa
katika Kamati ya PIC na kwa sasa anahamia Kamati ya PAC, Mhe. Ahmed Ally Salum
(Mb) ambaye alikuwa katika Kamati ya PAC na kwa sasa anahamia Kamati ya Huduma
na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Neema William Mgaya (Mb) ambaye alikuwa katika
Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na kwa sasa anahamia Kamati ya Ardhi,
Maliasili na Utalii pamoja na Mhe. Salma Mohamed Mwassa (Mb) ambaye alikuwa
katika Kamati ya Bajeti na kwa sasa anahamia Kamati ya Ardhi, Maliasili na
Utalii.
Taarifa inaeleza kuwa, Wajumbe waalikwa katika Kamati ni
pamoja na Mhe. Andrew John Chenge (Mb) ambaye yupo katika Kamati ya Sheria
Ndogo, Mhe. Joseph Roman Selasini (Mb) ambaye yupo katika Kamati ya LAAC, Mhe.
Dkt. Dalali Peter Kafumu (Mb) ambaye yupo katika Kamati ya Viwanda, Biashara na
Mazingira, Mhe. Japhet Ngalilonga Hasunga (Mb) ambaye yupo katika Kamati ya PAC,
Mhe. Albert Obama Ntabaliba (Mb) ambaye yupo katika Kamati ya PIC pamoja na
Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) ambaye yupo katika Kamati ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii.
Aidha, Walioondolewa katika Kamati ya Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge ni pamoja na Mhe. Dkt. Haji Hussein Mponda (Mb) pamoja na Mhe.
Najma Murtaza Giga, (Mb).
Wanaoteuliwa kuwa Wajumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na
Madaraka Ya Bunge ni pamoja na Mhe. Asha Abdalla Juma (Mb). Mhe. Emmanuel
Mwakasaka (Mb) pamoja na Mhe. Augustino Manyanda Masele (Mb).
No comments:
Post a Comment