Naibu Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson akiendesha kikao cha 36 cha
mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge na
Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa
kikao cha 36 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
Wageni mbalimbali
waliolitembelea Bunge wakifuatilia kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari St.
Anne Marie ya Mbezi Beach jijini Dar es salaam wakifuatilia kikao cha 36 cha
mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akijadiliana jambo
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki ndani ya
Ukumbi wa Bunge, Dodoma leo.
Baadhi ya Mawaziri Mawaziri
wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 36
cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
|
Naibu Waziri, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Sulemani Jafo
akijibu maswali ya wabunge wakati wa kikao cha 36 cha Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania leo.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akichangia jambo
kuhusu sekta ya Afya Bungeni mjini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwini Ngonyani akijibu maswali ya
wabunge kuhusu uboreshaji wa Mawasiliano ya simu vijijini Bungeni mjini Dodoma.
Wageni mbalimbali
waliolitembelea Bunge wakifuatilia kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Msanii maarufu wa
Muziki wa kizazi kipya Judith Wabura “Lady Jaydee” – (katikati) akiwa miongoni
wa wageni waliolitembelea Bunge kujionea shughuli za kikao cha 36 cha Bunge mjini
Dodoma leo.
Mbunge wa jimbo la
Mwibala (CCM) Mhe. Kangi Lugola akiomba mwongozo wa Spika wakati wa kikao cha
36 cha Bunge mjini Dodoma leo.
Msanii maarufu wa
Muziki wa kizazi kipya Judith Wabura “Lady Jaydee” – (kushoto) akisalimiana na
Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Mhe. Andrew Chenge
(Kulia) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
nje ya ukumbi wa Bunge.
Baadhi ya wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Mlowa iliyoko
Iringa Vijijini wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge wakiwa wameambatana na mwanafunzi
mwenzao Eva Tolage (16) wa pili kutoka kushoto aliyemwandikia Barua Rais Barack
Obama wa Marekani akiwa miongoni mwa vijana 2 kati ya 40,000 ambao barua zao
zilisomwa waliomtumia barua Rais huyo duniani kote kuomba viongozi wa dunia
kutekeleza ahadi zao kuhusu upatikanaji wa Maji chini ya Kampeni ya Simama na
EVA.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akimsalimia
Mwanafunzi Eva Tolage (16) kutoka Shule ya Sekondari Mlowa iliyoko Iringa Vijijini aliyemwandikia
Barua Rais Barack Obama wa Marekani akiwa miongoni mwa vijana 2 ambao barua zao
zilisomwa kati ya 40,000 kuomba viongozi wa dunia kutekeleza ahadi zao kuhusu
upatikanaji wa Maji chini ya Kampeni ya Simama na EVA.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano Mhe. Kassim Majaliwa akimsalimia Mwanafunzi Eliudi Sanyi wa
Shule ya Sekondari Mlowa iliyoko Iringa
Vijijini akimsalimia wa Tanzania nje ya ukumbi wa Bunge, Dodoma.
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Mlowa iliyoko
Iringa Vijijini ambao wako kwenye kampeni ya Simama na Eva, Mwanafunzi wa Shule
hiyo (katikati) aliyemwandikia Barua Rais Barack Obama wa Marekani kati ya
40,000 kuomba viongozi wa dunia kutekeleza ahadi kuhusu upatikanaji wa Maji.
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akisalimiana na Msanii wa kizazi kipya
Vanessa Mdee nje ya Ukumbi wa Bunge leo. Katikati ni Mhe. Januari Makamba,
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akizungumza jambo na Mhe. Januari Makamba,
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira nje ya Ukumbi wa Bunge,
Dodoma.Picha/Aron Msigwa –DODOMA.
No comments:
Post a Comment