WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, August 4, 2016

SPIKA WA BUNGE MHE NDUGAI ALIPOTEMBELEWA NA VIONGOZI MBALIMBALI NYUMBANI KWAKE BAADA YA KUREJEA NCHINI KUTOKA INDIA

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mke wa Spika Dkt Fatma Mganga. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka India ambapo alikwenda kwa ajili ya Matibabu


Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka India ambapo alikwenda kwa ajili ya uchunguzi wa Afya yake.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman aliyefika kumsalimia nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Spika amerejea nchini hivi karibuni kutoka India ambapo alikwenda kwa ajili ya uchunguzi pamoja na matibabu ya afya yake.




Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akifurahia jambo wakati akizungumza na Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim aliyemtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu.

Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akizungumza na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake.

Spika wa Baraza la wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid akisalimiana na Spika wa Bunge alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.

Spika Mstaafu Mhe Anne Makinda akizungumza na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai katikati akizungumza na baadhi ya Wabunge waliomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment