WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, September 8, 2016

MATUKIO KATIKA PICHA-BUNGENI LEO, KIKAO CHA TATU CHA MKUTANO WA NNE WA BUNGE LA KUMI NA MOJA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongea na wabunge na kuviasa vyama vya siasa vyenye tabia ya kufukuza wabunge kuacha hivyo kwani hatuwatendei haki wapiga kura na ni gharama kwa serikali

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akisalimiana na Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzania Bungeni na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe (MB) wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akijibu maswali ya wabunge wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.

Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzania na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe (MB) akimuuliza swali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) kuhusu hali ya uchumi nchini ambapo Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa alimhakikishia kuwa Serikali ipo imara katika  kusimamia  ipasavyo uchumi wa nchi.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba akijibu swali bungeni ambapo alisema serikali ipo katika mazungumzo na serikali ya China kwa ajili ya kuboresha zao la Tumbaku.

No comments:

Post a Comment