WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, September 7, 2016

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI LEO:KIKAO CHA PILI-MKUTANO WA NNE WA BUNGE LA KUMI NA MOJA

Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe.Margaret Sitta akimueleza Jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Mjini Dodoma.

Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali wakati wa kikao cha 2 cha bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alitoa wito kwa waajiri nchini kuwasilisha nyaraka za wastaafu kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii miezi mitatu hadi sita kabla ya kustaafu kwa wateja wao ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba Leo Bungeni Mjini Dodoma.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kintinku  mkoni Singida wakifuatili Kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Wazee na Wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama (MB) akimueleza jambo Mwansheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju leo Mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge akizungumza wakati akiongoza  kikao cha  pili cha Mkutano wa Nne wa  Bunge la Kumi na Moja.

No comments:

Post a Comment