WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, October 31, 2016

MHE SPIKA AKIZUNGUMZIA KUHUSU KUANZA KWA MKUTANO WA TANO WA BUNGEpika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma kuhusu kuanza kwa Mkutano wa Tano wa Bunge

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma kuhusu kuanza kwa Mkutano wa Tano wa Bunge

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Dodoma kuhusu kuanza kwa Mkutano wa Tano wa Bunge.
MHE SPIKA AZUNGUMZIA KUANZA KWA MKUTANO WA TANO WA BUNGE
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai ametangaza kuanza kwa vikao vya Mkutano wa Tano wa Bunge la 11 Mjini Dodoma kesho huku akitaja baadhi ya shughuli zitakazofanywa katika Mkutano huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Mjini Dodoma, Mheshimiwa  Spika alisema shughuli ya kwanza itakuwa ni Bunge kukaa kama Kamati ya Mipango kwa mujibu wa Kanuni ya 94 ya Kanuni za Kudumu za Bunge ili  kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Taofa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/ 2018.
Alisema katika mjadala huo wabunge watatoa ushauri kwa Serikali kuhusiana na vyanzo mbalimbali vya mapato na vipaumbele vya kuzingatia wakati Serikali ikiandaa bajeti ijayo.
“Mbali na shughuli hiyo vipindi vya Maswali na Majibu vitakuwepo kama kawaida ikiwemo kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu kinachokuwepo siku ya Alhamisi,” alisema Mhe Spika.
Alisema pia Katika Mkutano huu, Bunge litapokea Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na majibu ya Serikali kuhusiana na taarifa hiyo.
“Pia Bunge litajadili taarifa Taarifa ya Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Hesabu za Serikali Kuu na Serikali za Mitaa zilizokaguliwa kwa mwaka wa Fedha  2014/15 
“Vievile Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo itawasilisha taarifa yake bungeni kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo,” alisema 
Aidha, Mheshimiwa Spika alisema jumla ya miswada miwili ya sheria itajadiliwa na kupitishwa ambayo ni Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016(The Media Services Bill, 2016), na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 3 wa mwaka 2016 (The written Miscellaneous Amendments) (No. 3) Bill, 2016).
Alisema kutakuwepo na semina kwa wabunge wote kuhusu Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi katika Nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment