WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, October 17, 2016

VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE VYAANZA LEO MJINI DODOMA

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mheshimiwa Josephat Kandege akiongoza kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT) leo Mjini Dodoma .

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Juma Hamad Omar akisisitiza jambo katika kikao cha Kamati hiyo.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji akitoa ufafanuzi mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Bajeti kilichofanyika leo Mjini Dodoma

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakijadili jambo mara baada ya uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo iliyochukuliwa na Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka, Uchaguzi huo umefanyika leo Mjini Dodoma

Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akisikiliza maoni ya wajumbe wa Kamati hiyo katika kikao cha Kamati kilichofanyika leo Mjini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mheshimiwa Aeshi Hilary akichangia jambo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika leo Mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment