BUNGE kesho litafanya Kikao Maalum cha Bunge kwa
ajili ya kuuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa, Mheshimiwa Samuel
Sitta.
Akizungumzia kikao hicho Bungeni leo, Spika wa
Bunge Mheshimiwa Job Ndugai alisema kikao hicho ni cha kihistoria na kwamba
hakijawahi kutokea katika historia ya nchi.
Alisema mwili huo unataraijiwa kupokelewa na baadhi
ya wabunge katika uwanja wa Ndege Mjini Dodoma majira ya saa 8 mchana na
kuletwa Bungeni ambapo utaingizwa ndani ya Ukumbi wa Bunge.
“Wabunge mtapata nafsi ya kutoa salamu za
rambirambi na baadaye kutakuwa na utaratibu maalum wa kutoa heshima za mwisho
ambao tutaongozwa na Waziri Mkuu na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni,” alisema.
Alisema kutokana na muda kuwa mchache hakutakuwa na
zoezi la kuuga mwili mmoja mmoja na kwamba utaratibu uliondaliwa utaonyesha
heshima kubwa kwa Spika huyo mstaafu.
“Tutajenga msingi mzuri ambao viongozi wetu wa
kitaifa wakipatwa na jambo la namna hii watapata heshima hizo sio tu katika
uwanja wa Taifa Dar es Salaam au mahali popote lakini kwa kuletwa Bungeni
ambapo ndio nyumba ya wananchi wote wa Tanzania ilipo,” alisema.
Mheshimiwa Spika alisema baada ya shughuli hiyo
kukamilika mwili wa marehemu utasindikizwa hadi Uwanja wa Ndege kwa ajili ya
kusafirishwa kwenda Urambo Mkoani Tabora kwenye mazishi yanayotarajiwa
kufanyika keshokutwa.
Alisema Bunge litawakilishwa na wabunge kumi
watakaochaguliwa kwa kuzingatia uwakilishi wa vyama wakiongozwa na yeye
mwenyewe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira
na Watu wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama alitoa hoja ya kutengua
Kanuni ili kikao hicho maalum cha kumuaga Marehemu Samuel Sitta kiweze
kufanyika.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akisaini Kitabu cha Maombolezo cha Msiba wa Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta Bungeni Mjini Dodoma |
![]() |
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt Tulia Ackson akisaini Kitabu cha Maombolezo cha Msiba wa Spika
Mstaafu wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta Bungeni Mjini Dodoma.
|
Waheshimiwa Wabunge wakiendelea kusaini Kitabu
cha Mambolezo cha Msiba wa Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa Marehemu Samuel Sitta
Bungeni Mjini Dodoma.
|
Add caption |
No comments:
Post a Comment