WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, December 7, 2016

SPIKA NDUGAI AAHIDI KUDUMISHA USHIRIKIANO NA CPA-AFRIKA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akitoa hotuba ya kufunga mkutano wa Kamati Tendaji ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola-Kanda ya Afrika jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akizungumza na baadhi ya Wajumbe wa  wa Kamati Tendaji ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola-Kanda ya Afrika(CPA-AFRICA) jijini Dar es Salaam.Wakwanza kushoto ni Dkt. Acho Ihim Rais CPA-Afrika, Mhe Elijah Okupa Kaimu Mwekahazina wa CPA-Afrika na Mhe. Lindiwe Maseko Mwenyekiti wa kamati hiyo. Kamati hiyo ilikutana Jijini Dar es Salaam kwa muda wa wiki moja kujadili masuala mbalimbali yanayohusina na Chama hicho.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akitoa hotuba ya kufunga mkutano wa Kamati Tendaji ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola-Kanda ya Afrika jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola-Kanda ya Afrika (waliokaa) pamoja na Sekretarieti ya Chama hicho.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akiagana na Rais CPA-Afrika Dkt. Acho Ihim mara baada ya kufunga mkutano wa Chama hicho Jijini Dar es Salaam.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai ameahidi kudumisha ushirikiano na Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola-Kanda ya Afrika.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya chama hicho Mhe Ndugai amesema amekuwa Kiongozi na ameshiriki kwa muda mrefu katika shughuli za chama hicho na hivyo anaelewa mchango wa chama hicho katika kusaidia kusukuma mbele ajenda za Bara la Afrika katika Jumuiya ya Madola.
“Nipo pamoja nanyi na nimefanya kazi pamoja na Vingozi wengine katika Chama hiki katika kuzipeleka mbele ajenda za Bara la Afrika katika Jumuiya ya Madola,” alisema Mhe Ndugai.
Spika Ndugai aliongeza kuwa kwa kadri ambavyo Wabunge wapya wamekuwa wakichaguliwa ni vyema Wabunge wao wakaendelea kuelimishwa juu ya umuhimu wa Vyama vya Kibunge ikiwemo Chama cha Wabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola ili waweze kusaidia katika kusukuma mbele ajenda za bara la Afrika katika Vyama hivyo.
“Ninawahakikishia pia ushiriki wa Wabunge kutoka Bunge la Tanzania katika shughuli mbalimbali za chama hichi ikwemo Mkutano ujao wa 62 wa Chama cha Wabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola,” alisema Spika Ndugai.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati Tendaji wa CPA-Afrika Mhe Lindiwe Maseko alimshukuru Mhe Ndugai kwa ushirikiano ambao Bunge la Tanzania limeendelea kuonesha katika shughuli mbalimbali za CPA.
“Tunashukuru kwamba Tanzania imeendelea kuwa mwanachama hai wa CPA-Kanda ya Afrika na nimatumaini yetu kuwa mtaendelea kudumisha moyo huo,” alisema Mhe Maseko.
        

No comments:

Post a Comment