Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul
Makonda akihojiwa mbele ya ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kufuatia
wito wa Kamati hiyo kumtaka afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili
za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa
mapema mwezi februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau
Bunge.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda leo amehojiwa na Kamati ya Bunge ya
Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusiana na tuhuma za kuingilia haki, uhuru
na madaraka ya Bunge.
Mhe.
Makonda aliwasili Bungeni Dodoma majira ya saa nne asubuhi kuitikia wito
wa Kamati hiyo uliotokana na Azimio la Bunge lililotolewa na Bunge,
Februari 8, 2017 katika Kikao cha Nane cha Mkutano wa Sita wa Bunge
ambapo amehojiwa na kamati hiyo kwa muda wa masaa matatu kuhusu tuhuma zinazomkabili.
Katika
kikao hicho, Bunge liliazimia kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.
Makonda na Mkuu wa Mkoa wa Arumeru, Mhe. Alexander Mnyeti kuitwa mbele ya
Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge baada ya Bunge ili kujibu
tuhuma hizo.
Akizungumza
mara baada ya Kamati hiyo kumaliza kazi yake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya
Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. George Mkuchika alisema Kamati hiyo
imekutana leo baada ya kuagizwa na Mheshimiwa Spika wa Bunge kwa mujibu wa
Kanuni za Kudumu za Bunge.
“Tumefanya
kikao hiki cha Kamati baada ya kuagizwa na Mhe. Spika kwa kuwa kwa Mujibu wa
Kanuni zetu, Kamati hii inakutana pale tu inapoagizwa na Spika wa Bunge,”
alisema.
Alisema
Mhe. Spika aliiagiza Kamati hiyo imuite Mhe. Makonda mbele ya Kamati
kufuatia azimio hilo la Bunge lililopitishwa na Bunge Februari 8,
ambapo pamoja na mambo mengine Mkuu huyo wa Mkoa alitakiwa kufika mbele ya
Kamati kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.
Alisema
kwa mujibu wa Azimio hilo, Mhe. Makonda alidaiwa kutoa kauli kupitia
Televisheni ya Clouds akidai kwamba wabunge wanasinzia Bungeni jambo
lililoonekana kwamba ni kudharau Bunge.
“Napenda
kutoa taarifa kwamba Mhe. Makonda leo amekuja mbele ya Kamati na ametupa
ushirikiano mzuri, tumepokea maelezo yake na Kamati imemaliza kazi yake,”
alisema.
Alisema
kama ilivyo utaratibu, Kamati yake itakabidhi taarifa yake kwa Mhe. Spika kwa
mujibu wa Kanuni ambapo Spika ndiye atakaeamua namna ya kutoa raarifa kuhusu
kazi ya Kamati hiyo.
|
No comments:
Post a Comment