WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, June 23, 2017

SPIKA WA BUNGE AKABIDHI VITABU KWA SHULE TISA ZA SEKONDARI ZILIZOPO KONGWA, DODOMA

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai (katikati) akimkabidhi vitabu Makamu Mkuu wa  Shule ya sekondari Sejeli Ndg.Gerald Kagali. Spika Ndugai alikabidhi vitabu hivyo kwa shule tisa zilizopo Wilayani Kogwa, Dodoma ambapo  Vitabu hivyo ni msaada uliotolewa na Mtandao wa kuondoa Umasikini Nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao huo Ndg.  Mungwe Athuman




Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai  (kushoto) akishuhudia Mwenyeti wa Mtandao wa Kuondoa Umasikini Nchini, Ndg.Mungwe Athuman akimkabidhi kitabu Mwalimu mkuu wa  Shule ya Sekondari Banyibanyi Mwl.Grace Mbise.Kulia ni Meneja wa Mtandao huo Ndg. Peter Yobwa



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai  akizungumza na wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Banyibanyi iliyopo wilaya ya kongwa Mkoa wa Dodoma, baada ya kuwapatia vitabu vilivyotolewa na Mtandao wa Kuondoa Umasikini Nchini.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe  Job Ndugai (wa tatu kushoto waliosimama nyuma)katika  picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya sekondari Banyibanyi, baada ya kuwakabidhi vitabu.

No comments:

Post a Comment