WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, June 22, 2017

SPIKA APOKEA MSAADA WA VITABU 950 KUTOKA MTANDAO WA PEN.TRUST


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akipokea msaada wa vitabu kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Kuondoa Umasikini (PEN.TRUST),katikati ni Ndg. Mungwe Athman na kushoto ni Meneja wa Mtandao huo Ndg. Peter Yobwa.wanaoshuhudia tukio hilo nyuma ni Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge wakiongozwa na Ndg. Mussa Azzan Zungu(nyuma kulia). tukio lilimefanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akikata utepe ili aweze kufungua  boksi lenye vitabu alivyokabidhiwa na Mtandao wa Kuondoa Umasikini kwa ajili ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akionyesha moja ya kitabu alichokabidhiwa na Mtandao wa Kuondoa Umasikini kwa ajili ya Bunge, kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao huo Ndg. Mungwe Athman na kulia ni Mjumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge Mheshimiwa Peter Msigwa


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza baada ya makabidhiano ya vitabu kwa Bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Msaada uliotolewa na Mtandao wa Kuondoa Umasikini,.


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai  akisalimiana na  Mwenyekiti wa Mtandao wa kuondoa umasikini, Ndg. Mungwe Athman (kushoto)kabla ya Makabidhiano ya vitabu kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtandao huo, tukio lililofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment