Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tazania Mhe Job Ndugai
ameunda Kamati maalum ya Wabunge tisa itakayoshauri juu ya mfumo bora wa uchimbaji,
usimamizi, umiliki na udhibiti wa biashara
ya Madini ya Almasi hapa Nchini.
Kamati hiyo, itakuwa na wajumbe tisa
watakaoongozwa na Mwenyekiti wa Bunge Mheshimiwa Mussa
Zungu na itafanya kazi kwa siku 30.
Akizungumza kabla ya kuhitimisha shughuli za Bunge la Bajeti, Mheshimiwa Spika alisema ameunda kamati hiyo kupitia Waraka wa Spika namba 3 wa mwaka huu.
Akizungumza kabla ya kuhitimisha shughuli za Bunge la Bajeti, Mheshimiwa Spika alisema ameunda kamati hiyo kupitia Waraka wa Spika namba 3 wa mwaka huu.
“Kamati hii itatathmini mfumo wa
uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya almasi nchini kisha
kuandaa mapendekezo mahsusi kwa ajili ya kuishauri Serikali kuhusiana na
uendeshaji bora wa biashara ya madini hayo nchini,” alisema
Aliwataja wajumbe wa Kamati hiyo
kuwa ni Mbunge wa Viti maalum(chadema) Dk. Immaculate Sware Semesi,Mbunge wa
Viti maalum (CCM)Shally Raymond, Mbunge wa Tumbe Rashid Ali
Abdallah(CUF),Mbunge wa Iramba Mashariki Allan Kiula(CCM), Mbunge wa Viti
maalum(CCM) Restituta Mbogo, Mbunge wa Wawi Ahmed Juma Ngwali(CUF).
Wengine ni Mbunge wa Sumve Richard
Ndassa(CCM), Mbunge wa Tabora mjini Emmanuel Mwakasaka(CCM) na Mbunge wa Ilala
Mussa Zungu (CCM)ambaye atakuwa Mwenyekiti.
Alisema wajumbe hao
wameteuliwa kwa kuzingatia vigezo vya taaluma, uzoefu, pande za Muungano,
jinsia na uwakilishi wa Vyama vya Siasa Bungeni.
“Kamati hiyo itafanya kazi kwa muda wa siku thelathini kuanzia Julai 10, na Kituo Kikuu cha kazi kitakuwa katika Ofisi ya Bunge hapa Dodoma,”alisema
“Kamati hiyo itafanya kazi kwa muda wa siku thelathini kuanzia Julai 10, na Kituo Kikuu cha kazi kitakuwa katika Ofisi ya Bunge hapa Dodoma,”alisema
Aidha, alisema hadidu za rejea
za kamati hiyo ni Kuchambua Taarifa za Tume na Kamati mbalimbali zilizowahi
kuundwa na Serikali kwa ajili ya kushughulikia mfumo wa uchimbaji,
usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya almasi nchini na kuona Mapendekezo
yake na namna yalivyotekelezwa na Serikali.
Nyingine ni Kutathmini mfumo uliopo wa Uchimbaji, Usimamizi na Udhibiti wa biashara ya madini ya almasi nchini na kubainisha manufaa ambayo Serikali inapata kutokana na uwekezaji uliopo katika madini hayo na kubainisha na kushauri kuhusu utaratibu bora unaoweza kutumika katika kusimamia uwekezaji, uchimbaji na biashara ya madini ya almasi nchini,”alisema Spika Ndugai
“Hadidu nyingine ni kushughulikia jambo jingine lolote linalohusiana na mfumo wa uchimbaji, usimamizi na udhibiti wa madini ya almasi nchini,” alisema

Alisema kuundwa kwa Kamati hiyo
kumetokana na pendekezo la Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli la kuunda
Tume ya kuchunguza na kufuatilia madini ya alamasi alilolitoa Juni 12
mwaka huu alipohudhuria mkutano wa kupokea Taarifa ya Kamati yake ya Pili ya
Kuchunguza Masuala ya Kiuchumi na Kisheria kuhusu Usafirishaji wa Makinikia,
Kamati ya Prof. Nehemia Osoro).
Alisema Bunge liliahidi kutoa
ushirikiano wa dhati kwa kadri itakavyohitajika katika kuhakikisha kwamba
juhudi, uthubutu na uzalendo aliouonesha Rais katika kulinda rasilimali za
madini haupotei bure.
Hata hivyo alisema kuundwa kwa Kamati
hiyo ni hatua mojawapo ya utekelezaji wa Azimio la Bunge la kumpongeza Rais
Magufuli katika jitihada za kulinda rasilimali za Taifa.
“Tanzania ni miongoni mwa
wazalishaji wakubwa wa madini ya almasi duniani, Madini haya yana thamani na
umaarufu mkubwa katika biashara ya vito,kama ilivyo kwa dhahabu na madini
mengine ya thamani, yapo malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali nchini kwamba
hatujaweza kunufaika ipasavyo kutokana na wingi na thamani ya madini ya
almasi,”alisema Mheshimiwa Spika
Kamati hii itakayofuatilia kuhusu mfumo wa uchimbaji wa Madini ya Almasi hapa nchini ni ya pili kuudwa na Mhe Spika baada ya Kamati ile itayofuatilia suala la uchimbaji wa Madini ya Tanzanite hapa nchini ambayo pia aliuunda wakati wa mkutano wa Saba wa Bunge.
No comments:
Post a Comment