Mkutano
wa Saba wa Bunge umeahirishwa hadi Septemba 5 mwaka huu huku Spika wa Bunge
Mheshimiwa Job Ndugai akiwapongeza Wabunge na Mawaziri kwa ushirikianio wao
katika kipindi chote cha miezi mitatu.
Akitoa
shukrani hizo mara baada ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa kutoa hoja
ya kuahirisha Bunge, Mheshimiwa Spika aliwashukuru pia wasaidizi wake ambao ni
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson na wenyeviti wa tatu wa Bunge.
“Vilevile
kwa niaba ya wabunge wote, tunamshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kutuwezesha kuhakikisha Bunge hili linaendelea, Miswada
tunayoipitisha hapa anaipitisha kwa haraka bila kusita, tunaenedelea kufanya
kazi na Serikali yake ambayo iko hapa,” alisema
“Shukrani
kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye yupo hapa Bungeni, ametupa kila aina ya
ushirikiano, shukrani pia kwa mawaziri wote, Kambi Rasmi ya Upinzani kwa
changamoto mnazotupatia ambazo zimetusaidia kuendesha shughuli, shukrani kwa
Kamati ya Uongozi na Kamati nyingine zote” alisema.
Awali
akitoa hotuba ya kuahirisha Bunge, Mheshimiwa Majaliwa alisema Katika Mkutano
huu wa Bunge, Bunge lilijadili na kupitisha Bajeti za Wizara zote 19 pamoja na
Bajeti Kuu ya Serikali.
Aidha,
alisema Bunge limepitisha miswada mbalimbali pamoja na Maazimio matano ya
kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa na kwamba pia lilipitisha Azimio la
Bunge kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa hatua anazochukua za kukabiliana na
upotevu wa mapato ya Serikali katika Sekta ya Madini.
“Katika
Mkutano huu jumla ya maswali 499 ya msingi na mengine 1,834 ya nyongeza
yaliulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Serikali kupitia kwa
Waheshimiwa Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maswali ya papo kwa papo kwa Waziri
Mkuu,” alisema.
Alisema
pia Bunge liliendesha semina mbalimbalimbai kwa waheshimiwa Wabunge kwa lengo
la kuwajengea uwezo zaidi na kuwapa uelewa mpana wa masuala mbalimbali
yanayohusu maendeleo ya Nchi.
“Bunge
pia lilipata fursa ya kuchagua wawakilishi wa Tanzania kwenye Bunge la Jumuiya
ya Afrika Mashariki ambapo Wabunge tisa walichaguliwa
Aidha,
aliwataka Watanzania kuendelea kulinda na kudumisha amani nchini ili wananchi
waweze kushiriki shughuli za maendeleo bila hofu
Waziri
Mkuu pia alitumia fursa hiyo kuzungumzia maendeleo katika sekta mbalimbali
ikiwemo elimu, ulinzi na usalama, afya, ardhi pamoja na masuala mbalimbali
kuhusiana na Serikali za Mitaa
No comments:
Post a Comment