Spika
wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Balozi wa China nchini LU Youqing
anayemaliza muda wake alipofika kumuaga Ofisini kwake Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa masuala ya Diplomasia na Vyombo ya
Habari- Ubalozi wa China Bi. Wang Fang.
Balozi
wa China nchini LU Youqing anayemaliza muda wake akimueleza jambo Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai alipofika
kumuaga mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu
Mkurugenzi wa masuala ya Diplomasia na Vyombo ya Habari- Ubalozi wa China
Bi. Wang Fang.
Balozi
wa China nchini LU Youqing anayemaliza muda wake akimueleza jambo Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai alipofika
kumuaga mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu
Mkurugenzi wa masuala ya Diplomasia na Vyombo ya Habari- Ubalozi wa China
Bi. Wang Fang.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)
akimkabidhi zawadi Balozi wa China nchini LU Youqing anayemaliza
muda wake alipofika kumuaga mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es
Salaam.
Balozi
wa China nchini LU Youqing anayemaliza muda wake akimkabidhi zawadi
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai
alipofika kumuaga mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Katibu wa Spika Bw. Said Yakubu
Balozi
wa China nchini LU Youqing anayemaliza muda wake akimkabidhi zawadi
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai
alipofika kumuaga mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Katibu wa Spika Bw. Said Yakubu
Spika
wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai katika picha ya pamoja na Balozi wa China
nchini LU Youqing anayemaliza muda wake alipofika kumuaga Ofisini
kwake Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai akiagana na Balozi wa China nchini LU Youqing anayemaliza muda wake mara baada ya kuzungumza nae Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Na Lawrence Raphaely - Bunge
BALOZI wa China nchini LU Youqing amefika Ofisini kwa Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai Jijini Dar es Salaam mapema leo kumuaga baada
ya muda wake wa kukaa Tanzania kwisha.
Akizungumza na Spika Ndugai, Balozi huyo alisema kuwa muda
wake wa kutumikia kama Balozi wa China hapa nchini umekwisha hivyo hana budi
kuondoka ingawa angetamani kuendelea kubaki.
Balozi huyo aliongeza kuwa amefurahi kuona kuwa katika
kipindi chake chote akiwa hapa nchini uhusiano baina ya Tanzania na China
umezidi kukua.
“Ninafuraha kubwa wakati ninaporejea China kuona kuwa
uhusiano wetu wa kihistoria umezidi kukua na kwamba kuna ongezeko kubwa la
uwekezaji wa China hapa Tanzania na pia tumesaidia katika utekelezaji wa miradi
mingi,” alieleza Balozi huyo.
Balozi huyo ambaye amesema kuwa Tanzania ni nchi yake ya
mwisho kuhudumu kama Balozi aliongeza kuwa kwa sasa anarejea nchini China na
akiwa huko ataendelea kujitikita katika shughuli za kudumisha uhusiano baina ya
Tanzania na China.
“Tanzania ndiyo nchi yangu ya mwisho kuhudumu kama Balozi na nitakaporejea nyumbani
(China) nitaendelea kufanya shughuli nyingine ambazo zinalenga kuimarisha
uhusiano baina ya Tanzania na China,”
alisema Balozi Youqing.
Kutokana na hilo Balozi Youqing alisema kuwa ingawa anarejea nchini China lakini yupo tayari kwa
Tanzania kuendelea kumtumia kama Balozi wake katika utekelezaji wa shughuli
mbalimbali zitakozosaidia katika kudumisha ushirikiano baina wa nchi zote
mbili.
“Nipo tayari kwa Tanzania kuendelea kunitumia kama Balozi
wake aliyepo Nchini China, ninawakaribisha kwa mikono yote miwili tuendelee
kufanya kazi kwa pamoja,” alisema Balozi huyo.
Kwa upande wake Spika Ndugai alimshukuru Balozi huyo kwa kazi kubwa ambayo ameifanya
akiwa hapa nchini na kumueleza kuwa daima Watanzania wataendelea kumkumbuka kwa
kazi nzuri aliyoifanya.
“Mimi binafsi katika kipindi chako ukiwa kama Balozi
nimeshuhudia ongezeko kubwa la watanzania wengi tena wa hali ya chini
wakisaifiri kwenda China kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kibiashara,”
alisema Spika Ndugai na kuonegeza kuwa; kupitia fursa hiyo Watanzania wengi
wameweza kujiajiri kupitia biashara ya kununua bidhaa toka China na kuja kuuza
hapa nchini.
Mhe Spika pia alimshukuru Balozi Youqing kwa uchakapakazi
wake katika kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia
wataalamu kutoka nchini China.
“Unaondoka lakini utakapojisikia kurudi, sisi kama Bunge na
Serikali kwa ujumla tupo tayari kukupokea kwa mikono miwili na kuendelea
kufanya kazi na wewe,” alisema Spika Ndugai.
Mbali na hayo Spika Ndugai pia alimuomba Balozi Youqing
kuendelea kuwa Balozi wa Tanzania atakaporejea nchini China kwa kuendelea
kufanya shughuli ambazo zitasaidia katika kuimarisha ushirikiano baina ya pande
zote mbili.
No comments:
Post a Comment