Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Rais wa Umoja wa
Mabunge ya Afrika ambaye pia ni Spika wa Bunge la Guine-Bissau Mheshimiwa
Cipriano Cassama Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Spika huyo wa Guine-Bissau
alitembelea Mhe Ndugai kwa lengo la kumpa mwaliko wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wa kujiunga na Umoja
wa Mabunge ya Africa (African Parliamentary
Union). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja huo Mheshimiwa N’ZI Koffi.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akipokea mwaliko wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa
kujiunga na Umoja wa Mabunge ya Africa (African
Parliamentary Union) kutoka kwa Rais
wa Umoja huo ambaye pia ni Spika wa Bunge la Guine-Bissau Mheshimiwa Cipriano
Cassama Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja huo Mheshimiwa. N’ZI Koffi.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) katika picha
ya pamoja na Rais wa Umoja wa Mabunge ya Africa (African Parliamentary Union) ambaye pia ni Spika wa Bunge la
Guine-Bissau Mheshimiwa Cipriano Cassama (kushoto) na Katibu Mkuu wa Umoja huo Mheshimiwa. N’ZI Koffi (kulia).

Rais wa Umoja wa Mabunge ya Africa (African Parliamentary Union) ambaye pia
ni Spika wa Bunge la Guine-Bissau Mheshimiwa Cipriano Cassama (kushoto)
akimkabidhi zawadi Spika wa Bunge Mhe Job
Ndugai (kulia) mara baada ya mazungumzo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es
Salaam.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati)
akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mara baada ya kupokea mwaliko
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kujiunga na Umoja wa Mabunge ya
Africa (African Parliamentary Union)
Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Na Lawrence Raphaely - Bunge
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepokea mwaliko wa kujiunga
na Umoja wa Mabunge ya Afrika (African Parliamentary Union).
Mwaliko huo uliwasilishwa na Rais wa Umoja huo ambaye pia ni Spika wa Bunge la Guine-Bissau Mheshimiwa Cipriano Cassama.
Akipokea mwaliko huo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai alisema ameupokea mwaliko huo kwa mikono miwili na kwamba ataufanyia kazi.
Spika Ndugai amepokea mwaliko huo punde baada ya kurejea nchini hii leo ambapo alikuwa nje ya nchi kwa takribani mwezi mmoja akifanya ziara ya Kibunge katika nchi mbalimbali.
Awali Mheshimiwa Spika Ndugai alihudhuria katika Mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika uliofanyika Mjini Abuja ambapo katika mkutano huo alichaguliwa Mwenyekiti wa Maspika na Viongozi wa Bunge katika Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika.
Kwa wadhifa huo, Mhe Ndugai ataongoza Maspika wenzake toka Mabunge na Mabaraza ya kutunga Sheria 63 yaliyoko katika nchi 18 za Jumuiya ya Madola kwenye Bara la Afrika.
Aidha mara baada ya Mkutano huo Spika Ndugai alitembelea Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu na kufanya mazungumzo na Spika mwenzake, Mhe Dr Amal Al Qubaisi ambapo aliwasilisha mapendekezo rasmi ya kuanzisha Urafiki wa Kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu.
Mbali na hayo Mhe Ndugai kwa niaba ya Maspika wa Afrika alihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais wa 12 wa Iran ambapo kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo, Rais huapishwa Bungeni na Spika.
Baada ya hafla hiyo Mhe. Spika Job Ndugai alipata wasaa wa kukutana na Spika wa Bunge la Iran, Mhe. Dkt. Ali Larijani na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuimarisha mahusiano ya kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Iran
Kwa upande mwingine akiwa mjini Tehran, Iran Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai alikutana na kufanya mazungumzo na Rais mpya wa Iran, Mheshimiwa Hassan Rouhani ambapo Mheshimiwa Spika alimpongeza kwa kuchaguliwa kwake kwa mara ya pili na kumuahidi ushirikiano wa karibu baina ya Bunge la Tanzania na lile la Iran.
Spika Ndugai amrejea nchini wakati baadhi ya Kamati za Bunge zimeshaanza kukutana huku nyingine zikitarajiwa pia kuanza vikao kuanzia wiki ijayo kabla ya kuanza kwa Mkutano nane wa Bunge ambao umepangwa kuanza Septemba 05, 2017.

No comments:
Post a Comment