WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, August 2, 2017

MHE. SPIKA ATEMBELEA BUNGE LA UMOJA WA FALME ZA KIARABU

 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai ametembelela Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu lililopo Abu Dhabi na kufanya mazungumzo  na Spika wa Bunge hilo, Mhe. Dkt. Amal Al Qubaisi ambapo amewasilisha  mapendekezo rasmi ya kuanzisha umoja na urafiki wa kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu.Mapendekezo hayo yamekubaliwa

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Spika wa Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Dkt. Amal Al Qubaisi baada ya kutembelea Bunge hilo na kufanya nae mazungumzo ambapo pia amewasilisha  mapendekezo rasmi ya kuanzisha umoja na urafiki wa kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu


Mhe. Spika Job Ndugai akikasaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu  huku akiangaliwa na Spika wa Bunge hilo, Mh. Dkt. Amal Al Qubaisi (katikati) na Katibu wa Bunge Ndg. Ahmed Shabeeb
Mhe. Spika Job Ndugai akikabidhi ujumbe wake maalum kwa  Spika wa Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu, Mh. Dkt. Amal Al Qubaisi.


Mhe. Spika Job Ndugai akipewa maelezo kutoka kwa  Spika wa Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhr. Dkt. Amal Al Qubaisi wakati alipotembelea Bunge hilo .



No comments:

Post a Comment