WAJUMBE WA CPA TAWI LA TANZANIA WAKUTANA NA WAJUMBE WA CPA TAWI LA CANADA JIJINI DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la
Tanzania Dkt Raphael Chegeni (katikati) akiongoza kikao wakati Wajumbe wa
Kamati hiyo walipokutana na Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola
Tawi la Canada katika Ofisi Ndogo za
Bunge Jijini Dar es Salaam mapema leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi
la Canada Mhe. Yasmin Ratansi (wa kwanza
kushoto) akisisitiza jambo wakati Wajumbe wa Chama hicho kutoka Canada
walipokutana na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la
Tanzania katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam mapema leo
Mwenyekiti
wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge,
Mhe. Yasmin Ratansi akimkabidhizawadi Mwenyekiti
wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge
ya Jumuiya ya Madola Tawi la Tanzania Dkt Raphael Chegeni mara baada ya Wajumbe
wa pande zote mbili kuzungumza mapema leo katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini
Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati
Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya
ya Madola Tawi la Tanzania katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Chama
cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada mara baada ya mazungumzo katika
Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment