WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, October 19, 2017

KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI YAENDELEA NA VIKAO MJINI DODOMA

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI, Mheshimiwa Salma Kikwete akichangia jambo katika kikao cha Kamati hiyo. Katikakati ni Katibu wa Kamati hiyo, Happiness Ndalu na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Daniel Mtuka. Kikao hicho kimefanyika Mjini Dodoma leo ambapo wamejadili Taarifa ya Bohari ya Dawa (MSD) na Taarifa ya Mpango wa Taifa wa kudhibiti

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi wakiwa katika kikao  na Watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambapo walikuwa wakipokea Taarifa ya Bohari ya Dawa (MSD) na Taarifa ya Mpango wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI. Kikao hicho kimefanyika Mjini Dodoma.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Faustine Ndugulile akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizotolewa na wajumbe wa Kamati ya Masuala ya Ukimwi katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Mjini Dodoma, kushoto Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu  na kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizarani, Dkt. Neema Rusibamayila.

Wajumbe wa Kamati ya Masuala ya UKIMWI wakiendelea na kikao

No comments:

Post a Comment