Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai
(kushoto)akizungumza na Spika wa Bunge la Kuwait, Mheshimiwa Marzouq Al
Ghanim (kulia) kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa 137 wa Umoja wa Mabunge
Duniani uliofanyika leo katika Jiji la St. Petersburg, Urusi. Kushoto kwake
ni Mbunge wa Kigoma kaskazini, Mheshimiwa Peter Serukamba na anaefuata ni
Katibu wa Spika, Ndg. Said Yakubu
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai
(wa pili kushoto)akizungumza na Spika wa Bunge la Burundi, Mheshimiwa
Pasc Nyabenda (wa pili kulia) kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa 137 wa Umoja
wa Mabunge Duniani uliofanyika leo katika Jiji la St. Petersburg, Urusi.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job
Ndugai akipiga kura ya kumchagua Rais wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) wakati
wa Mkutano wa 137 wa Umoja wa Chama cha Mabunge Duniani unaoendelea Jijini St
Petersburg,Urusi. Nyuma yake ni Mbunge wa Kigoma kaskazini, Mheshimiwa Peter
Serukamba na Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Susan Lyimo.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai
(wa pili kulia)katika mazungumzo na Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Urusi
na kiongozi wa Bunge la nchi hiyo, Komredi Gennady Zyuganov (wa pili kushoto)
alipomtembelea leo ofisini kwake katika maadhimisho ya miaka 100 ya Mapinduzi
Makuu ya Urusi. Mheshimiwa Spika yupo nchini Urusi, akishiriki Mkutano wa 137
wa Chama cha Mabunge Duniani unaoendelea leo Jijini St. Petersburg, Urusi
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai
(kushoto) akimkabidhi zawadi Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Urusi na
kiongozi wa Bunge la nchi hiyo Komredi Gennady Zyuganov (katikati)
alipomtembelea ofisini kwake. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini huko, Jenerali
Mstaafu Wynjones kisamba. Mheshimiwa Spika yupo nchini humo kushiriki mkutano
wa 137 wa Chama cha Mabunge Duniani.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai
(kushoto) akivishwa nishani maalum ya maadhimisho ya miaka 100 ya Mapinduzi
Makuu ya Urusi na Kiongozi wa Chama cha kikomunisti cha Urusi, Komredi Gennady
Zyuganov ambae ni Kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Urusi na kiongozi wa
Bunge la nchi hiyo alipomtembelea ofisini kwake. Mheshimiwa Spika yupo nchini
humo akishiriki Mkutano wa 137 wa Chama cha Mabunge Duniani.
No comments:
Post a Comment