WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, October 9, 2017

KATIBU MPYA WA BUNGE AAPISHWA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai leo  Ikulu Jijini Dar es Slaam kuchukua nafasi ya aliyekuwa Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai mara baada ya kumuapisha leo  Ikulu Jijini Dar es Slaam kuchukua nafasi ya aliyekuwa Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli (kulia) akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) wakati wa hafla ya kuapisha Mawaziri, Manaibu Waziri na Katibu wa Bunge Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai ambaye ameapishwa leo kuchukua nafasi ya Dkt. Thomas Kashililah.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli  (kulia) akizungumza na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) wakati wa hafla ya kuapisha Mawaziri, Manaibu Waziri na Katibu wa Bunge Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai ambaye amepishwa leo kuchukua nafasi ya Dkt. Thomas Kashililah.



Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (kulia) akiteta jambo na Katibu wa Bunge aliyeapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam Ndg. Stephen Kagaigai (kushoto).

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Katibu wa Bunge aliyeapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam Ndg. Stephen Kigaigai (kushoto) na kulia  ni aliyekuwa Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah.

No comments:

Post a Comment