Thursday, November 30, 2017
Friday, November 24, 2017
Thursday, November 16, 2017
Wednesday, November 15, 2017
WAHARIRI NA WAANDISHI WA MAGAZETI MATATU WAHOJIWA MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA MAADILI KWA KOSA LA KUTOA TAARIFA ZINAZOHUSU USHAHIDI NA MWENENDO WA KIKAO CHA KAMATI HIYO BILA KUPATA IDHINI YA BUNGE
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mtanzania Bw. Denis
Msacky akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Nipashe
kwa kosa la kutoa taarifa zinazohusu
ushahidi na mwenendo wa kikao cha Kamati
hiyo bila kupata idhini ya Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34
(1) (f) na (g) ya Sheria ya Kinga,
Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
Mhariri/Mwandishi wa Habari Gazeti la
Mtanzania Bw. Bakari Kimwaga akiapaa kabla ya kuanza akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge Nipashe kwa kosa la kutoa
taarifa zinazohusu ushahidi na mwenendo wa kikao cha Kamati hiyo bila kupata idhini ya
Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f) na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki
za Bunge, Sura ya 296.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi Bw. Angetile Osiah na Mwanasheria wake mbele ya Kamati
ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Nipashe kwa kosa la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na
mwenendo wa kikao cha Kamati hiyo bila
kupata idhini ya Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34 (1)
(f) na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka
na Haki za Bunge, Sura ya 296.
Mhariri wa Gazeti la Nipashe Bw. Edmond
Msangi akijieleza mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Nipashe
kwa kosa la kutoa taarifa zinazohusu
ushahidi na mwenendo wa kikao cha Kamati
hiyo bila kupata idhini ya Bunge kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34
(1) (f) na (g) ya Sheria ya Kinga,
Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296.
Na Debora Sanja
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imewahoji wahariri
pamoja Waandishi wa Habari wa Magazeti ya Mtanzania, Mwananchi na Nipashe kwa kosa
la kutoa taarifa zinazohusu ushahidi na
mwenendo wa kikao cha Kamati hiyo bila
kupata idhini ya Bunge.
Akizungumza mara baada ya kuwahoji mashahidi hao, Mwenyekiti
wa Kamati hiyo, Mhe. Almasi Athuman
Maige (Mb) alisema wahusika wote walifika mbele ya Kamati na kujibu
tuhuma hizo ambazo ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f) na (g) ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki
za Bunge, Sura ya 296.
Mheshimiwa Maige alisema Kamati baada ya kuwasikiliza mashahidi
wote waliofika itaandaa Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge,
Mheshimiwa Job Ndugai.
“Kanuni zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii
zinazofanywa zitabakia kuwa ni siri hadi hapo itakapomaliza kazi yake na
kuwasilisha taarifa Bungeni,” alisema.
Aliwataja waliofika katika Kamati hiyo kuwa ni Ndugu Denis
Msaki ambaye ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania na mwandishi wake Ndugu
Bakari Kimwanga, Ndugu Edmond Msangi Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe na
mwandishi wake Ndugu Gwamaka Alipipi na Ndugu Angetile Osiah Mhariri Mtendaji
wa gazeti la Mwananchi na Mwandishi wake
Ndugu Elias Msuya.
SPIKA NDUGAI APOKEA TAARIFA YA MKUTANO WA BUNGE LA AFRIKA ULIOFANYIKA KUANZIA TAREHE 6 MPAKA 20 OKTOBA, 2017 NCHINI AFRIKA YA KUSINI
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)
akizungumza na Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Bunge la
Tanzania katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. wa pili
kushoto ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania, Mhe. Asha Juma, wa pili kulia ni
Mjumbe Mhe. Stephen Masele na kulia ni Mjumbe Mhe. David Silinde.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akipokea taarifa ya Mkutano wa Bunge la Afrika uliofanyika kuanzia tarehe 6 mpaka 20 Oktoba, 2017 nchini Afrika ya kusini, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Asha Juma (wa pili kulia) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. kushoto ni Mjumbe, Mhe. Stephen Masele na kulia ni Mjumbe, Mhe. David Silinde
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akipokea taarifa ya Mkutano wa Bunge la Afrika uliofanyika kuanzia tarehe 6 mpaka 20 Oktoba, 2017 nchini Afrika ya kusini, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Asha Juma (wa pili kulia) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma. kushoto ni Mjumbe, Mhe. Stephen Masele na kulia ni Mjumbe, Mhe. David Silinde
Thursday, November 9, 2017
Monday, November 6, 2017
NAIBU SPIKA DKT. TULIA KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA CHAMA CHA JUMUIYA YA MADOLA UNAOFANYIKA MJINI DHAKA, BANGALADESH.
Sunday, November 5, 2017
WAJUMBE WA KAMATI TATU ZA BUNGE WAKIWA KATIKA SEMINA MJINI DODOMA
Ndugu Seraphine
Tamba akitoa mada kuhusu Mchakato wa Utungaji Sheria katika Semina ya Wabunge
wa Kamati ya Kamati ya Katiba na Sheria, Kamati ya Sheria Ndogo na Kamati Mambo
Nje, Ulinzi na Usalama.
|
Baadhi ya
Wajumbe wa Kamati za Bunge zilizoshiriki Semina kuhusu Mchakato wa Utungaji
Sheria wakifuatilia mada katika Semina iliyofanyika Mjini Dodoma.
|
Subscribe to:
Posts (Atom)