Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwatambulisha Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Tanzania wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Kimichezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ukumbi wa Sabasaba Jijini, Dar es Salaam
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (watatu toka kulia) katika picha ya pamoja na Wageni wa meza kuu wakati wa ufunguzi huoWaheshimiwa Wabunge wa Tanzania wakifanya usajili wakati wa ufunguzi huo
Washiriki wa Mashindano ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ni Waheshimiwa Wabunge na Watumishi wa Mabunge hayo wakifuatilia ufunguzi wa Mashindano hayo Jijini Dar es Salaam |
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (wa tano toka kulia mstari wa mbele) akiongoza Wageni waalikwa na Wachezaji wa Timu za Bunge la Tanzania na Burundi kuimba nyimbo ya Taifa ya Mataifa yao kabla ya kuanza kwa mechi baina ya timu hizo Uwanja wa Taifa ikiwa ni sehemu ya mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwasalimia wachezaji wa Timu ya Bunge la Burundi kabla ya kuanza kwa mechi yao na Timu ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwasalimia wachezaji wa Timu ya Bunge la Tanzania kabla ya kuanza kwa mechi yao na Timu ya Burundi ikiwa ni sehemu ya mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki |
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiteta jambo na Kocha wa
Timu ya Bunge la Tanzania Mhe. Venance Mwamoto kabla ya kuanza kwa
mechi kati ya Timu ya Bunge la Tanzania na Burundi katika Uwanja wa
Taifa Jijini Dar
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson akiwasalimia wachezaji wa Timu ya Bunge la Tanzania kabla ya kuanza kwa mechi yao na Timu ya Burundi ikiwa ni sehemu ya mashindano ya Mabunge ya Afrika Mashariki |
Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Bunge la
Tanzania na Burundi (hawapo pichani) kabla ya kuanza kwa mechi
baina ya timu hizo Uwanja wa Taifa ikiwa ni sehemu ya mashindano ya
Mabunge ya Afrika Mashariki
Kikosi cha Bunge la Tanzania |
Kikosi cha Bunge la Burundi
Na Debora Sanja-Bunge
Spika wa Bunge,
Mheshimiwa Job Ndugai amefungua mashindano ya Nane ya Mabunge ya Nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki huku akisisitiza michezo hiyo kudumisha umoja na
ushirikiano katika Jumuiya hiyo.
Akizungumza katika
ufunguzi wa michezo hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Sabasaba Jijini Dar
es Salaaam alisema mbali na michezo kuimarisha afya lakini pia inadumisha umoja
baina ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Tutumie michezo
hii kudumisha ushirikiano uliopo ndani ya Nchi za Afrika Mashariki ili uzidi
kuwa na nguvu na Umoja huu uwe mfano kwa Nchi nyingine za Afrika,” alisema.
Alisema Tanzania
ikiwa mwenyeji wa Mashindano hayo imejipanga kuhakikisha yanafanyika na
kumalizika kwa usalama kwa kuwa hali ya Ulinzi na Usalama imeimarishwa.
Aidha,
alisema Timu za Bunge za Tanzania zimejiandaa kisawasawa kuchukua ushindi
katika michezo yote.
Kwa upande wake
Spika wa Bunge la Seneti la Burundi, Mheshimiwa Reverien Ndikuriyo alishukuru
kwa mapokezi mazuri kutoka Tanzania na kusisitiza pia kudumisha umoja katika
michezo hiyo.
Awali akitoa
maelezo ya mashindano hayo, Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai alisema
michezo hiyo imeshirikisha Nchi nne za Uganda, Burundi, Kenya na Tanzania
pamoja na Timu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Alisema Nchi za
Rwanda na Sudan ya Kusini wameomba udhuru wa kutoshiriki mashindano haya kwa
mwaka huu.
Naye Mwenyekiti wa
Timu ya Bunge, Mheshimiwa William Ngeleja aliitaja michezo itakayochezwa katika
mashindano hayo kuwa ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, mpira
wa pete, riadha, kuvuta kamba na gofu.
Baadhi ya viongozi
wengine waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge
la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge la Kenya, Mheshimiwa Moses
Cheboi, Kiongozi wa Upinzani kutoka Bunge la Uganda, mabalozi na viongozi wa
vyombo vya ulinzi na usalama.
Mara baada ya
uzinduzi kulifanyika mchezo wa riadha na kuvuta kamba ambapo katika mchezo wa
riadha Timu ya Wanawake ya Bunge la Tanzania iling’ara huku kwa wanaume
Timu ya Kenya iliongoza.
Kwa upande wa Kuvuta
Kamba Timu ya wanaume ya Tanzania iliibuka na ushindi huku wanawake ilishinda
Timu ya Kenya.
- Waziri Mkuu awaasa Wchezaji
Mheshimiwa
Majaliwa ametoa Rai hiyo wakati
akifungua mashindano ya Mpira wa Miguu katika Tanzania na Burundi yaliyofanyika
katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Alisema pamoja na
kwamba kila nchi inahitaji ushindi lakini inapokuwa inatafuta ushindi huo
iangalia jinsi gani inawapa Watanzania Burudani kwa kuzingatia viango hivyo vya
‘Fair Play’.
“Leo tunaanza
mashindano ya Mpira wa Miguu, najua kila nchi inahitaji ushindi lakini hata
hivyo tunangalie burudani tunayowapa Watanzania, tuangalie Sheria za FIFA za
‘Fair Play’, kila mtu aendelee kucheza bila dosari na ninawatakia mchezo mwema
kila mmoja apate amafanikio,” alisema.
Waziri Mkuu alisema
nchi zote zinashiriki mashindano hayo ni ndugu hivyo ni vema wakayatumia
katika kuimarisha ushirikiano wa Mabunge ya Jumuiya hiyo.
Katika ufunguzi huo
Waziri Mkuu aliambatana na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mheshimiwa Dkt.
Tulia Ackson, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt.
Harrison Mwakyembe pamoja na Katibu wa Bunge la Tanzania Stephen Kagaigai.
Katika mechi ya kwa
kwanza timu ya Bunge la Tanzania imeibuka kidedea baada ya kuibamiza
magoli matatu (3) kwa mawili (2) Timu ya Bunge la Burundi.
- Sambamba na hilo ,
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa
Salma Kikwete (Mb) ,amewataka wachezaji wa Timu za Mabunge ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki wanaposhiriki mashindano hayo wazingatie kwamba michezo ni afya.
Mama Salma ametoa kauli hiyo wakati akifungua
mashindano ya Mpira wa Wavu kwa Timu za wanaume za Bunge la Kenya na Tanzania.
Alisema mbali na burudani lakini pia
wachezaji watambue kwamba michezo ni afya hivyo wajitokeze kwa wingi kushirii
mashindano hayo kwa ajili ya kuimarisha afya zao.
“Mnashiriki mashindano haya, naomba mtambue
kuwa mbali na burudani, pia michezo ni afya, undugu na unadumisha uyshirikiano
hivyo ni vizuri tukiidumisha,’ alisema.
Katika mchezo huo Timu ya Bunge la Kenya
iliibuka mshindi kwa kuifunga Timu ya Bunge la Tanzania kwa seti 3 – 1.
No comments:
Post a Comment