WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, April 5, 2019

KATIBU WA BUNGE ATEMBELEWA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA CAMEROON JIJINI DODOMA

Katibu wa Bunge ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Ndg. Stephen Kagaigai akizungumza jambo na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Nchi za Jumuiya ya Madola Kimataifa Mhe. Emilia Monjowa Lifaka alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo.

Katibu wa Bunge la ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Ndg. Stephen Kagaigai akimuelezea jambo Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Nchi za Jumuiya ya Madola Kimataifa Mhe. Emilia Monjowa Lifaka alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya UtendajI ya Jumuiya hiyo Mhe. Maria Kangoye. 

Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Nchi za Jumuiya ya Madola Kimataifa Mhe. Emilia Monjowa Lifaka akimuelezea jambo Katibu wa Bunge ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Ndg. Stephen Kagaigai alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo. 

Katibu wa Bunge ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Ndg. Stephen Kagaigai pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Nchi za Jumuiya ya Madola Kimataifa Mhe. Emilia Monjowa Lifaka wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jumuiya hiyo walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma hii leo. Kulia ni Mhe. Jitu Soni na kushoto ni Mhe. Maria Kangoye

No comments:

Post a Comment