WABUNGE WAHUDHURIA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA TANAPA NA HIFADHI YA NGORONGORO WILAYANI SERENGETI
Makamu
wa Rais, Mhe. Samia Suluhu akimkabidhi Mwenyekiti wa Wabunge Walemavu na wadau
wa Utalii Mhe. Riziki Lulida Cheti cha Utambulisho wa kutambua mchango wa
Wabunge hao kwenye Sekta ya Utalii nchini wakati wamaadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Hifadhi
za Taifa Tanzania (TANAPA) na eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenye Viwanja vya
Fort Ikoma Wilayani Serengeti hii leo.
Wabunge
wanaounda Umoja wa Wabunge wenye Ulemavu nchini pamoja na Wabunge wengine
wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu na baadhi ya
mawaziri kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania
(TANAPA) na eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenye Viwanja vya Fort Ikoma
Wilayani Serengeti hii leo.
Wabunge
wanaounda Umoja wa Wabunge wenye Ulemavu Tanzania wakiwa na wawakilishi wengine
wa makundi ya Walemavu wakionyesha Vyeti walivyotunukiwa na Makamu wa Rais Mhe.
Samia Suluhu kwa kutambua mchango wao kwenye sekta ya Utalii hapa nchini wakati
wa Maadhimisho ya miaka 60 ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na
eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenye Viwanja vya Fort Ikoma Wilayani Serengeti
hii leo.
No comments:
Post a Comment