Mtaalam mwezeshaji kutoka Shirika la
Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) Ndg. Charles Meshack akielezea jambo
kwenye mafunzo yalitolewa kuwajengea uwezo Wabunge juu ya ya Usimamizi bora wa
misitu ya asili nchini.
Mkurugenzi wa Wakala wa Misitu Tanzania ((TFS) Prof. Dos Santos Silayo akielezea jambo
kwenye mafunzo yalitolewa kuwajengea uwezo Wabunge juu ya ya Usimamizi bora wa
misitu ya asili nchini.
MHESHIMIWA ZUNGU AFUNGUA MAFUNZO KWA WABUNGE KUHUSU USIMAMIZI WA MISITU YA ASILI NCHINI
|
Wabunge
wanaounda Chama cha Wabunge Marafiki wa Mazingira (TAPAFE) wamepewa mafunzo ya
kuwajengea uwezo wabunge juu ya usimamizi bora wa misitu ya asili iliyomo
nchini.
Akizungumza
katika mafunzo hayo Mgeni rasmi ambaye ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,
Mheshimiwa Mussa Zungu alisema kutokana na kutoweka kwa kasi kwa misitu mingi
ya asili, Wizara yake inalo jukumu kubwa kuhakikisha hali hiyo inadhibitiwa kwa
kushirikiana na wananchi.
Aidha,
Mheshimiwa Zungu alitoa wito kwa wananchi kujikita kwenye matumizi ya nishati
mbadala ikiwemo Gesi na Makaa ya mawe ili kukabiliana na upotevu mkubwa wa
misitu ya asili na kuepusha uchafuzi wa mazingira unaotokana na hewa ukaa
ambayo huzalishwa na kuni na mkaa.
Alisema
“pamoja na juhudi zote zinazofanywa na
Serikali ya awamu ya tano, Wadau wa maendeleo pamoja na Sekta binafsi, wananchi
tuna wajibu wa kushirikiana na wadau hawa ili kukomesha uharibifu wa misitu kwa
kujikita kwenye matumizi ya nishati mbadala”
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Wabunge wanaounda Chama cha Wabunge Marafiki wa
Mazingira (TAPAFE) Mheshimiwa Jitu Soni alimhakikishia Mheshimiwa Waziri kuwa
Chama hicho kiko tayari kusaidiana na Serikali kutoa elimu sehemu mbalimbali
nchini juu ya umuhimu wa kuhifadhi misitu.
Naye
mtaalam mwezeshaji kutoka Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) Ndg.
Charles Meshack alisema, kati ya hekta milioni 22 za ardhi zilizoko chini ya
Vijiji ni hekta milioni 2 pekee ndizo zinazohifadhiwa na mamlaka za Serikali na
hivyo kufanya sehemu kubwa ya ardhi ya Vijiji kuwa hatarini kuharibiwa.
Akichangia
mada katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Prof.
Dos Santos Silayo alisema takwimu zinaonyesha kuwa Serikali inapoteza mapato ya
shilingi bilioni 200 kila mwaka kutokana na kukosekana kwa usimamizi wa misitu
iliyo chini ya mamlaka za Vijiji huku hekta laki 4 za misitu zikitoweka kila
mwaka sambamba na hilo.
Mafunzo
hayo yaliyohudhuriwa na Wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati za Ardhi, Maliasili
na Utalii na Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira yalifanyika kwenye Ukumbi
wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma hii leo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment