Watumishi wa Kitengo
cha TEHAMA wa Ofisi ya Bunge wakipatiwa mafunzo kuhusu mfumo wa Kadi ya Tathimini
na Uwajibikaji wa Malaria kutoka kwa Ndugu Khalifa Munisi. Mafunzo hayo
yameandaliwa na Umoja wa Wabunge walio katika Mapambano dhidi ya Malaria
(TAPAMA) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kupitia Programu ya Taifa ya
Kupambana na Kutokomeza Malaria pamoja na Sekretarieti ya Maraisi na Viongozi
wa Afrika walioungana kupambana na Malaria. Lengo la kuwajengea uwezo watumishi
wa kitengo hicho ili waweze kuiwasaidia wabunge kutumia Kadi hiyo kupitia
kwenye vishikwambi (‘tablet’) vyao.
|
Mafunzo yakiendelea katika Ukumbi wa Msekwa B
|
|
Mafunzo yakiendelea
|
No comments:
Post a Comment