Mratibu wa Mradi wa Panda Miti Kibiashara (PFP) Ndg. Rahel Swai akitoa taarifa na maelezo kuhusu mradi huo kwa Waheshimiwa wabunge kabla ya kufanya ziara na kuona mradi huo.
Kamishna Uhifadhi wa TFS Prof. Dos Silayo akitoa taarifa kwa waheshimiwa wabunge ya Shamba la Miti Sao Hill kabla ya kufanya ukaguzi wa shamba hilo. Na Zanele Chiza Iringa. |
Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. Aloyce Kwezi ametoa pongezi
wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na maeneo
yanayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambapo amesema
hatua hiyo imesaidia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa idadi ya wanyama.
“Napongeza kazi kubwa iliyofanywa na Wizara, TANAPA wamefanya
kazi kubwa sana ya kupunguza ujangili, hili limesaidia kuongezeka kwa idadi ya
wanyamapori hapa nchini, pia nawapongeza TFS kwa kazi kubwa ambayo wamefanya”
Amesema Dkt. Kwezi
Kuhusu uboreshaji wa miundombinu maeneo ya Hifadhi, Kamati
hiyo imeishauri Wizara katika kipindi hiki cha bajeti kufuatilia kwa karibu
ujenzi wa Barabara inayotoka Iringa kuelekea katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
No comments:
Post a Comment