Katibu wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemteua Bi. Nenelwa Mwihambi kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Bi. Mwihambi anachukua nafasi ya aliyekuwa Katibu wa Bunge, Bw. Stephen Kagaigai ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kabla ya kuteuliwa kuwa katibu wa Bunge Bi. Mwihambi alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge.
Aidha, Bi. Mwihambi anakuwa Mwanamke wa kwanza kuteuliwa kuwa Katibu wa Bunge.
No comments:
Post a Comment