WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, February 7, 2022

KAMATI YA KILIMO YAPOKEA TAARIFA YA WIZARA KUHUSU MPANGO MKAKATI KUELEKEA TIJA NA MAGEUZI YA SEKTA YA KILIMO



1.       Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji , Mhe. Christine Ishengoma akizungumza mara baada ya kamati hiyo kupokea Taarifa ya Wizara ya Kilimo kuhusu Mpango Mkakati wa kuelekea Tija na Mageuzi ya Sekta ya Kilimo.  




       Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakati Wizara yake ilipowasilisha wa Taarifa kuhusu Mpango Mkakati wa kuelekea Tija na Mageuzi ya Sekta ya Kilimo.

 


Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Kilimo Ndg. Gungu Mibavu  akiwasilisha Taarifa kuhusu Mpango Mkakati wa kuelekea Tija na Mageuzi ya Sekta ya Kilimo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji.





Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao  wa Wizara ya Kilimo Ndg. Chinyagu Nyasebwa  akiwasilisha Taarifa  ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kuelekea Tija na Mageuzi ya Sekta ya Kilimo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji. 
 

                                               
 

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe na Naibu waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde wakiteta jambo wakati Wizara yao ilipofika mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na kuwasilisha Taarifa kuhusu Mpango Mkakati wa kuelekea Tija na Mageuzi ya Sekta ya Kilimo. 

   Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji  Mhe. Bashiru Ally na Mhe JaneJelly Ntate wakifuatilia uwasilishaji wa Taarifa ya Wizara ya Kilimo kuhusu Mpango Mkakati wa kuelekea Tija na Mageuzi ya Sekta ya Kilimo. 


No comments:

Post a Comment