Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Azan Zungu akiapa
mara baada ya kuwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa kura 296 kati ya kura 301 zilizopigwa na Waheshimiwa Wabunge walikuwepo
Bungeni.
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson Bungeni Jijini
Dodoma akimkabidhi vitendea kazi Naibu Spika wa Bunge Mhe. Mussa Azan Zungu
mara baad ya kumuapisha Bungeni.
Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Azan Zungu akipongezwa mara
baada ya kuapishwa kuwa Naibu Spika wa Bunge.
Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Azan Zungu akizungumza
mara baada ya kuapishwa kuwa Naibu Spika wa Bunge.
Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Azan Zungu amechaguliwa kuwa Naibu Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kura 296 kati ya kura 301
zilizopigwa na Waheshimiwa Wabunge walikuwepo Bungeni.
Mara baada ya kuchaguliwa Mhe. Zungu aliapishwa na Spika wa Bunge, Mhe.
Dkt. Tulia Ackson Bungeni Jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kuapishwa Mhe. Zungu aliwashukuru Waheshimiwa
Wabunge na Chama chake cha Mapinduzi kikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Samia
Suluhu Hassan kwa kumpendekeza na hatimaye kuchaguliwa kushika nafasi hiyo.
Aidha, Mhe. Zungu ameahidi
kushirikiana na Waheshimiwa Wabunge kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujenga
Taifa.
No comments:
Post a Comment