Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mhe. Grace Tendega akizungumza wakati Kamati hiyo ilipofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa kuzungumza naye kabla ya kuanza ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo Mkoani humo
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Grace Tendega wakiwasili katika Halmashauri Mji Mafinga kukagua miradi ya maendeleo
Wajumbe wa Kamati ya LAAC wakikagua mradi wa ujenzi wa fremu za biashara katika Halmashauri ya Mji Mafinga
------------------------------------------
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wamewashauri Watendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga kuhakikisha kuwa wanamipango dhabiti ambayo itawasaidia katika kutekeleza miradi ya kuwaingizia mapato.
Kamati hiyo ilitembelea Halmashauri hiyo kwa ajili ya kukagua ufanisi uliopo katika Ujenzi wa Maegesho ya Malori katika Eneo la Sabasaba na Ujenzi wa Fremu katika Soko la Mafinga.
Akizungumza mara baada ya kukagua miradi hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Grace Tendega (Mb) aliungana na Wajumbe wengine katika kuipongeza Halmashauri hiyo kwa ujenzi wa miradi hiyo ambayo itawasaidia katika kuongeza mapato lakini akawashauri kuhakikisha kuwa wanamipango dhabiti katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Aliongeza kuwa ni vyema wahakikishe kwamba miradi wanayoanzisha wanaikamilisha kabla ya kuanzisha miradi mipya.
Kamati ya LAAC kundi la kwanza iliwasili Mkoani Iringa hii leo kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo inayosimamiwa na mamlaka na Serikali za Mitaa ambapo kesho wataendelea na ziara hiyo katika Mkoa wa Njombe kabla ya kuelekea Mkoa wa Mbeya.
Kwa upande mwingine kundi la pili la Kamati ya LAAC linafanya ziara kama hiyo katika Mikoa ya Shinyanga na Mwanza.
ReplyForward |
No comments:
Post a Comment