WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, March 28, 2022

KAMATI YA PAC IMEKAGUA MRADI WA MAJI MKURANGA UNAOTEKELEZWA NA DAWASA


Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) tenki la maji lililopo Mkuranga wakati wajumbe hao walipotembelea DAWASA na kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Mkuranga
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Japhet Hasunga akibonyeza kitufe cha kuwashia pampu ya maji  wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Mkuranga unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiangalia tenki la maji lililopo Mkuranga wakati wajumbe hao walipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa maji wa Mkuranga unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

No comments:

Post a Comment