Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo na watendaji wa Bohari ya Dawa (MSD) wakati Kamati hiyo ilipokagua kiwanda cha kutengeneza barakoa, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Brig.Jen.Dkt. Gabriel Mhidize, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekhalage Na kulia ni Katibu wa Kamati Erick Maseke
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Brig.Jen.Dkt. Gabriel Mhidize akizungumza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kabla ya wajumbe hao hawajangia ndani ya Kiwanda cha kutengeneza dawa cha Keko wakati Kamati hiyo ilipotembelea MSD na kukagua kiwanda hicho na Kiwanda cha kutengeneza barakoa
Afisa Udhibiti Ubora kutoka Bohari ya Dawa (MSD), akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) jinsi mashine ya kutengeneza barakoa inavyofanya kazi wakati Kamati hiyo ilipotembelea MSD na kukagua kiwanda hicho na Kiwanda cha kutengeneza dawa cha Keko
No comments:
Post a Comment