Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imewasili mkoani Arusha kwa ajili ya Ziara ya siku 3, mkoani humo na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Eng. Richard Ruyango.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Mhe. Jerry Silaa akitambulisha Kamati yake kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Eng. Richard Ruyango (kulia) wakati kamati hiyo ilipokwenda kusalimia Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa PIC Mhe. George Malima.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Mhe. Jerry Silaa akizungumza jambo wakati Kamati yake Kamati yake ilipokwenda kusalimia Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huo. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Eng. Richard Ruyango.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Eng. Richard Ruyango akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakati Kamati hiyo ilipoenda kusalimia kwa Mkuu wa Mkoani huo.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakisikiliza wakati Kamati hiyo ilipokwenda kusalimia Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha .
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Eng. Richard Ruyango wakati Kamati hiyo ilipokwenda kusalimia Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha .
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakisikiliza wakati Kamati hiyo ilipokwenda kusalimia Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha .
KAMATI YA PIC KUFANYA ZIARA YA SIKU TATU YA UKAGUZI WA MIRADI MKOANI ARUSHA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imewasili mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya siku 3, mkoani humo.
Baada ya kuwasili Jijini Arusha Kamati ilikwenda kujitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Eng. Richard Ruyango ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.
Akizungumzia ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya PIC, Mhe. Jerry Silaa amesema Kamati hiyo ipo Mkoani Arusha kwa ajili ya kutembelea na kukagua miradi ambayo Serikali imewekeza fedha za Umma.
Mhe. Silaa ameitaja Miradi hiyo kuwa ni Uboreshaji wa Miundombinu katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), kukagua miradi ya Uboreshaji wa huduma za maji na Usafi wa mazingira inayotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWASA).
Mhe. Silaa ametaja mradi mwingine kuwa ni ule wa uwekezaji katika Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu Tanzania(TPHA).
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Eng. Ruyango ameikaribisha Kamati ya PIC na kuihakikishia ushirikiano wa Serikali katika utekelezaji wa majukumu yake.
Aidha, ameihakikishia kamati kuwa Mkoa wa Arusha uko salama.
No comments:
Post a Comment