WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Sunday, March 13, 2022

KAMATI YA PAC YAKAGUA MRADI WA MAJI IKUNGI

 

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singinda, Mhe. Jerry Muro akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesebu za Serikali (PAC) wakati Kamati hiyo ilipowasili katika eneo la mradi wa maji Ikungi unaotekelezwa na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA). Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka ipo Mkoani Singinda kufanya ziara ya ufuatiliaji wa fedha za umma katika miradi mbalimbali

Mwenyekiti wa Kamati Kamati ya Bunge ya Hesebu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akieleza jambo wakati Kamati hiyo ilipotembelea eneo la mradi wa maji Ikungi unaotekelezwa na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA). Kamati hiyo ipo Mkoani Singinda kufanya ziara ya ufuatiliaji wa fedha za umma katika miradi mbalimbali.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesebu za Serikali (PAC) wakimsikiliza Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Singida, Lucas Said akielezea utekelezaji wa mradi wa maji Ikungi wakati Kamati ilipotembelea na kukagua mradi huo. Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka ipo Mkoani Singinda kufanya ziara ya ufuatiliaji wa fedha za umma katika miradi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment