WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, May 20, 2022

NAIBU SPIKA ZUNGU AKUTANA NA SPIKA MSTAAFU WA BUNGE LA KENYA BUNGENI JIJINI DODOMA.

Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), akimpokea Spika Mstaafu wa Bunge la Kenya, Mhe. Francis Ole Kaparo alipomtembelea leo tarehe 20 Mei, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.


Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), akizungumza na Spika Mstaafu wa Bunge la Kenya, Mhe. Francis Ole Kaparo alipomtembelea leo tarehe 20 Mei, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.


Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), akiambatana na mgeni wake ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Kenya, Mhe. Francis Ole Kaparo (katikati) pamoja na Mke wa Spika huyo, Mhe. Sarah Paulata (kushoto) wakiwa katika ukumbi wa Bunge kushuhudia kipindi cha maswali na majibu wakati wa Kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa Saba leo tarehe 20 Mei, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.


Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), pamoja na Spika Mstaafu wa Bunge la Kenya, Mhe. Francis Ole Kaparo (wapili kushoto mbele) pamoja na Mke wa Spika huyo Mstaafu, Mhe. Sarah Paulata (wapili kulia mbele) wakishuhudia kipindi cha maswali na majibu wakati wa Kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa Saba leo tarehe 20 Mei, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), pamoja na mgeni wake Spika Mstaafu wa Bunge la Kenya, Mhe. Francis Ole Kaparo wakitambulishwa wakati wa Mkutano wa Saba Kikao cha Ishirini na Saba leo tarehe 20 Mei, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.



 Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), akizungumza na mgeni wake ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Kenya, Mhe. Francis Ole Kaparo (katikati) pamoja na Mke wa Spika huyo Mstaafu, Mhe. Sarah Paulata (kulia) baada ya kushuhudia kipindi cha maswali na majibu wakati wa Kikao cha Ishirini na Saba cha Mkutano wa Saba leo tarehe 20 Mei, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.

Friday, May 13, 2022

SPIKA DKT. TULIA ACKSON AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAIMU POSTAMASTA MKUU BUNGENI JIJINI DODOMA



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akizungumza na Kaimu Postamasta Mkuu, Ndg. Macrice Mbodo alipomtembelea leo Mei 13, 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akizungumza na Kaimu Postamasta Mkuu, Ndg. Macrice Mbodo (katikati) alipomtembelea leo Mei 13, 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Meneja wa Posta Mkoa wa Dodoma, Ndg. Ferdinand Kabyemela



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Postamasta Mkuu, Ndg. Macrice Mbodo alipomtembelea leo Mei 13, 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Thursday, May 12, 2022

SPIKA DKT. TULIA AONGOZA KIKAO CHA MAJADILIANO NA VIONGOZI WA VYAMA VYA HIARI VYA WABUNGE JIJI DODOMA



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson (Mb), akiongoza kikao cha majadiliano na viongozi wa vyama vya hiari vya Wabunge leo Mei 11, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu na Kulia ni Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc

Viongozi wa vyama vya hiari vya Wabunge wakiwa katika kikao cha majadiliano yaliyoongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson (Mb), leo Mei 11, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Wabunge walio katika Mapambano dhidi ya Rushwa (APNAC) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Mhe. Kapteni. George Mkuchika akichangia jambo wakati wa kikao cha majadiliano ya viongozi wa vyama vya hiari vya Wabunge yaliyoongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson (Mb), leo Mei 11, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. 

Tuesday, May 10, 2022

SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU MNADHIMU WA KWANZA WA SERIKALI BUNGENI KUTOKA BUNGE LA GHANA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akizungumza na Naibu Mnadhimu wa Kwanza wa Serikali Bungeni kutoka Bunge la Ghana, Mhe. Habib Iddrissu (katikati) na Naibu Mnadhimu Mkuu wa kambi ya walio wachache kutoka Bunge la Ghana, Mhe. Ahmed Ibrahim pale ugeni kutoka Bunge hilo ulipomtembelea leo ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, Mei 10, 2022


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akizungumza na ugeni kutoka Bunge la Ghana ukiongozwa na Naibu Mnadhimu wa Kwanza wa Serikali Bungeni, Mhe. Habib Iddrissu (kulia kwake) ulipomtembelea leo ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, Mei 10, 2022


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), katika picha ya pamoja na Naibu Mnadhimu wa Kwanza wa Serikali Bungeni kutoka Bunge la Ghana, Mhe. Habib Iddrissu (kulia) alipomtembelea leo ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, Mei 10, 2022



 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati), katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Bunge la Ghana ukiongozwa na Naibu Mnadhimu wa Kwanza wa Serikali Bungeni, Mhe. Habib Iddrissu (kulia kwake) ulipomtembelea leo ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma, Mei 10, 2022