WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, October 31, 2023

MKUTANO WA KUMI NA TATU WA BUNGE WAANZA JIJINI DODOMA

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) akiingia Bungeni kwa ajili ya kuongoza Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) akimuapisha Mbunge wa Mbarali Mheshimiwa Bahati Kenneth Ndingo wakati wa Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge
Mbunge wa Mbarali Mheshimiwa Bahati Kenneth Ndingo akila kiapo cha Uaminifu
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) akizungumza wakati wa Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge
Waheshimiwa Wabunge wakiimba Wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge

 Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge umeanza Jijini Dodoma ambapo shughuli ya kwanza katika Kikao cha Kwanza cha Mkutano Mkutano huo ilikuwa ni Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) kumuapisha Mheshimiwa Bahati Kenneth Ndingo ambaye alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbarali kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Marehemu Francis Mtega.

Aidha, katika Mkutano huu Bunge linatarajia kujadili na kupitisha Maazimio yafuatayo;

Azimio la Bunge la Kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mb, kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Mkataba wa Kuanzisha Taasisi ya Dawa ya Afrika la Mwaka 2023 (Treaty for Establishment of the African Medicines Agency – AMA).

Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya Tanzania Kuridhia Kujiunga na Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu la Mwaka 2009 (Statute of the International Renewable Energy Agency – IRENA).

Kwa upande mwingine  katika Mkutano huu Bunge linatarajia kujadili Miswada ifuatayo;

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.4) wa Mwaka 2023 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.4) Bill, 2023] .

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Sekta ya Sheria wa Mwaka 2023 [The Legal Sector Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2023].

Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote wa Mwaka 2023

Mbali na hayo katika Mkutano huu Bunge linatarajia kupokea na kujadili taarifa za Kamati za PAC na LAAC kuhusu Hesabu zilizokaguliwa na CAG kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 na Taarifa ya Kamati ya PIC kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

Katika Mkutano huu Bunge pia linatarajia kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.

                                ------------------------------------------------------------------


 

No comments:

Post a Comment