WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Saturday, April 2, 2016

KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE YAKUTANA KUTATHIMINI KAZI ZA KAMATI ZA BUNGE

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiteta jambo na Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati cha Kamati ya Uongozi ya Bunge leo tarehe 2/42016 Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.Kamati hiyo inayojumuisha Wenyeviti wote wa Kamati za Kudumu za Bunge ilikutana ili kufanya thathmini ya shughuli za kamati za Kudumu za Bunge kabla ya Serikali kuwasilisha Mapendekezo ya Mpango na ukomo wa Bajeti ya mwaka 2016/17 wiki ijayo.

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha Kamati cha Kamati ya Uongozi ya Bunge. Kamati hiyo inayojumuisha Wenyeviti wote wa Kamati za Kudumu za Bunge ilikutana ili kufanya thathmini ya shughuli za kamati za Kudumu za Bunge kabla ya Serikali kuwasilisha Mapendekezo ya Mpango na ukomo wa Bajeti ya mwaka 2016/17 wiki ijayo.
(Picha zote na Ofisi ya Bunge)

WABUNGE BARANI AFRIKA WAKUTANA NA KUJADILI NAMNA NCHI ZA AFRIKA ZINAVYOWEZA KUPINGA BIASHARA HARAMU YA SILAHA.

Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwahutubia baadhi ya Wabunge kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakati wa Mkutano wa kujadili namna gani nchi za Afrika zinavyoweza kupinga biashara haramu ya silaha, leo Jijini Dar es Salaam.


Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Ramadhani Mwinyi akiwahutubia baadhi ya Wabunge kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakati wa Mkutano wa kujadili namna gani nchi za Afrika zinavyoweza kupinga biashara haramu ya silaha, leo Jijini Dar es Salaam.
Mratibu kutoka Umoja wa Mataifa Bwana Alvaro Rodriguez akiwahutubia baadhi ya Wabunge kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakati wa Mkutano wa kujadili namna gani nchi za Afrika zinavyoweza kupinga biashara haramu ya silaha, leo Jijini Dar es Salaam.

Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akiongea na Mkurugenzi wa Taasisi ya Parliamentarians for Global Action (PG) Bwana Peter Barcroft (kushoto) kabla ya kuanza kwa mkutano wa siku mbili (2-3Aprili, 2016) kujadili juu ya namna gani nchi za Afrika zinavyoweza kupinga biashara haramu ya silaha, oleo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mbunge aliyemaliza muda wake na Mwanasheria, Mhe. Pindi Chana.


Baadhi ya Wabunge kutoka Afrika Mashariki, Magharibi na Kusini wakifuatilia mada katika mkutano huo uliohusu namna gani nchi za Afrika zinavyoweza kupinga biashara haramu ya silaha, leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Ofisi ya Bunge)