WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, June 3, 2016

MATUKIO BUNGENI LEO TAREHE 3 JUNI, 2016


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson akiendesha kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.


Baadhi ya Wabunge na Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 36 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.


Wageni mbalimbali waliolitembelea Bunge wakifuatilia kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.

Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari St. Anne Marie ya Mbezi Beach jijini Dar es salaam wakifuatilia kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akijadiliana jambo na Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki ndani ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma leo.


Baadhi ya Mawaziri Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 36 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Sulemani Jafo akijibu maswali ya wabunge wakati wa kikao cha 36 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akichangia jambo kuhusu sekta ya Afya Bungeni mjini Dodoma leo.


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwini Ngonyani akijibu maswali ya wabunge kuhusu uboreshaji wa Mawasiliano ya simu vijijini Bungeni mjini Dodoma.


Wageni mbalimbali waliolitembelea Bunge wakifuatilia kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.


Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Judith Wabura “Lady Jaydee” – (katikati) akiwa miongoni wa wageni waliolitembelea Bunge kujionea shughuli za kikao cha 36 cha Bunge mjini Dodoma leo.


Mbunge wa jimbo la Mwibala (CCM) Mhe. Kangi Lugola akiomba mwongozo wa Spika wakati wa kikao cha 36 cha Bunge mjini Dodoma leo.


Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Judith Wabura “Lady Jaydee” – (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Mhe. Andrew Chenge (Kulia) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi nje ya ukumbi wa Bunge.


Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari  Mlowa iliyoko Iringa Vijijini wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge wakiwa wameambatana na mwanafunzi mwenzao Eva Tolage (16) wa pili kutoka kushoto aliyemwandikia Barua Rais Barack Obama wa Marekani akiwa miongoni mwa vijana 2 kati ya 40,000 ambao barua zao zilisomwa waliomtumia barua Rais huyo duniani kote kuomba viongozi wa dunia kutekeleza ahadi zao kuhusu upatikanaji wa Maji chini ya Kampeni ya Simama na EVA.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akimsalimia Mwanafunzi Eva Tolage (16) kutoka Shule ya Sekondari  Mlowa iliyoko Iringa Vijijini aliyemwandikia Barua Rais Barack Obama wa Marekani akiwa miongoni mwa vijana 2 ambao barua zao zilisomwa kati ya 40,000 kuomba viongozi wa dunia kutekeleza ahadi zao kuhusu upatikanaji wa Maji chini ya Kampeni ya Simama na EVA.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Kassim Majaliwa akimsalimia Mwanafunzi Eliudi Sanyi wa Shule ya Sekondari  Mlowa iliyoko Iringa Vijijini akimsalimia wa Tanzania nje ya ukumbi wa Bunge, Dodoma.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari  Mlowa iliyoko Iringa Vijijini ambao wako kwenye kampeni ya Simama na Eva, Mwanafunzi wa Shule hiyo (katikati) aliyemwandikia Barua Rais Barack Obama wa Marekani kati ya 40,000 kuomba viongozi wa dunia kutekeleza ahadi  kuhusu upatikanaji wa Maji.


Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akisalimiana na Msanii wa kizazi kipya Vanessa Mdee nje ya Ukumbi wa Bunge leo. Katikati ni Mhe. Januari Makamba, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.



Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akizungumza jambo na Mhe. Januari Makamba, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira nje ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma.Picha/Aron Msigwa –DODOMA.

Thursday, June 2, 2016

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI LEO JUNI 2 ,2016.

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto), Mhe. Margaret Sitta Mbunge wa Urambo (katikati) na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge kuhudhuria kikao cha 35 cha Bunge.
 Baadhi ya Waheshimiwa wabunge wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge kuhudhuria kikao cha 35 cha mkutano wa 3 leo mjini Dodoma.
 Baadhi ya Waheshimiwa wabunge wakiingia ndani ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson akiongoza kikao cha 35 cha Mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
 Mchezaji wa kulipwa wa mpira wa kikapu nchini Marekani kutoka Tanzania, Hasheem Thabeet (kulia) akiwa na wageni mbalimbali waliolitembelea Bunge wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge leo.
 Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akichangia jambo  wakati wa kikao cha 35 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
 Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni akijibu maswali ya wabunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni Dodoma.
 Baadhi ya Wabunge na Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 35 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson (kulia) akisalimiana na Meneja wa VETA mkoa wa Iringa Bw. Maganga nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.Katikati ni Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson (kulia) akizungumza jambo na Meneja wa VETA mkoa wa Iringa Bw. Maganga (kushoto) na Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
 Mchezaji wa kulipwa wa mpira wa kikapu nchini Marekani kutoka Tanzania Hasheem Thabeet (kushoto) akifurahia jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju (wa pili kutoka kushoto) na baadhi ya Wabunge nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Haki , Maadili na Madaraka ya Bunge na Mbunge wa Newala Mhe. George Mkuchika (katikati) akizungumza jambo na Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Peter Msigwa nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma.Kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsisitiza jambo Meneja wa VETA mkoa wa Iringa  Bw. Maganga nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma.
 Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Venance Mwamoto (wa pili kutoka kulia), , Mhe. Livingstone Lusinde (wa tatu kutoka kulia) na Mhe. Joseph Kasheku Msukuma ( pili kutoka kushoto)wakifurahia jambo  na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe nje ya Ukumbi wa Bunge leo.
 Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto (wa pili kutoka kulia), Mbunge wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde (wa tatu kutoka kulia) na Mbunge wa Geita vijijini Mhe. Joseph Kasheku Msukuma ( pili kutoka kushoto)wakimweleza jambo Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe nje ya Ukumbi wa Bunge leo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Kulia) akizungumza jambo na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni leo mjini Dodoma.
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson (kulia) akifungua mafunzo ya Wabunge kuhusu uelewa wa dhana ya Ufisadi yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wataalam wa Kuchunguza mianya ya Ufisadi yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Msekwa, Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia mafunzo kuhusu uelewa wa dhana ya Ufisadi yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wataalam wa Kuchunguza mianya ya Ufisadi yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Dodoma.

Picha na Aron Msigwa na Fatma Salum–MAELEZO, DODOMA.

Wednesday, June 1, 2016

MATUKIO KATIKA PICHA BUNGENI LEO, JUNI 1, 2016.



 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha 34 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ndani ya Ukumbi wa Bunge kabla ya kuanza kwa kikao cha 34 cha Mkutano wa 3 wa Bunge mjini Dodoma.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Moga iliyoko jijini Dar es salaam wakifuatilia shughuli za kikao cha 34 cha Bunge mjini Dodoma. Wanafunzi 90 wa shule hiyo wamelitembelea Bunge hilo kujifunza namna linavyoendeshwa.
 Baadhi ya Mawaziri na Wabunge wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 34 mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Malisili na Utalii Mhe.Mhandisi Ramo Makani akijibu maswali ya Wabunge yaliyoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa kipindi cha Maswali na majibu leo, Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Muhagama akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa Serikali ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 leo mjini Dodoma. Wizara hiyo inaliomba Bunge lipitishe kiasi cha shilingi Trilioni 8.7 kwa ajiri ya matumizi ya kawaida na matumizi mengine.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji wakiandika maoni ya Wabunge waliokuwa wakichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara Fedha na Mipango kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 leo mjini Dodoma.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kulia) akimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina nje ya Ukumbi wa Bunge leo.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa(kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto nje ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma.
 Baadhi ya Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari Moga iliyoko jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge kufuatilia shughuli za kikao cha 34.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kulia) kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma.