WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, March 24, 2017

SPIKA WA BUNGE AFUNGA MKUTANO WA 72 WA CPA KANDA YA AFRIKA

Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge Wanachama Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA Africa Region ) Bw. Demetrius Mgalami akimuelezea jambo  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 72 wa Kamati Tendaji ya CPA Afrika Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika kusini Mhe Lindiwe Maseko ( wa pili kushoto) na Katibu wa Chama cha  CPA Afrika ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania   Dkt Thomas Kashililah.


Wajumbe wa Kamati Tendaji ya CPA Afrika  wakiimba wimbo wa Jumuiya hiyo kabla ya kuanza kwa Mkutano huo.


Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Wajumbe wa Kamati Tendaji CPA Kanda ya nAfrika  wakati wa Mkutano wa Chama hicho uliofanyika Jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Viongozi wa Kamati hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya CPA Afrika ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Lindiwe Maseko akizungumza wakati wa Mkutano huo.



Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (kulia waliokaa mbele) ambaye pia ni Mwenyejiti wa Bodi ya Chama cha CPA Afrika akiongoza kikao cha Bodi hiyo mara baada ya kikao cha Kamati Tendaji ya chama hicho kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya CPA Mhe. Lindiwe Maseko. Wengine katika picha ni Wajumbe wa Bodi hiyo.

SPIKA WA BUNGE ALIPOENDA KUHANI MSIBA WA MAREHEMU Sir GEORGE KAHAMA


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akimsalimia Mama Jannet Kahama, Mjane wa Marehemu Sir George Kahama alipokwenda kuhani Msiba nyumbani kwa marehemu Mikocheni, Dar es Salaam.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akimsalimia Mama Jannet Kahama, Mjane wa Marehemu Sir George Kahama alipokwenda kuhani Msiba nyumbani kwa marehemu Mikocheni, Dar es Salaam
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akisaini kitabu cha Waombolezaji wakati alipokwenda kuhani Msiba nyumbani kwa marehemu Mikocheni, Dar es Salaam.


Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Mama Jannet Kahama, Mjane wa Marehemu Sir George Kahama alipokwenda kuhani Msiba nyumbani kwa marehemu Mikocheni,  Dar es Salaam.

Wednesday, March 8, 2017

TAARIFA KUHUSU VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE


Kamati ya Bunge yatua Loliondo kusaka suluhu



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imefanya ziara katika  katika Pori Tengefu la Loliondo ili kujionea  hali hailisi ya mgogogro  wa muda mrefu katika pori hilo kwa kutembelea baadhi ya maeneo muhimu ambayo ndio hutajwa kama kiini cha mgogoro huo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mheshimiwa Muhandisi Atashasta  Nditiye anasema wamejionea walicho kiona na wataishauri serikali ipasavyo ili iweze kutoa maamuzi sahihi ili kumaliza mvutano wa muda mrefu katika eneo hilo
Mheshimiwa Mhandisi Nditiye amesema wajumbe wa kamati hiyo, wamefanikiwa kupita sehemu kubwa ya eneo hilo, ambalo linapendekezwa kugawanywa ili kutengwa eneo la kilomita 1500 kwa ajili ya uhifadhi wa ikolojia ya Serengeti.
Akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati hiyo, Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Serengeti, William Mwakilema alisema kwa manufaa yaTaifa na dunia ni muhimu kutengwa eneo la kilomita 1500 ili lihifadhiwe.
Alisema eneo hilo ambalo ni mapito ya nyumbu kutoka hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya, hadi Serengeti na baadaye hifadhi ya Ngorongoro pia ndio eneo la mazalia ya nyumbu na vyanzo vya maji, limeharibiwa sana na mifugo na shughuli za kibinaadamu na lisipo hifadhiwa uhai wa Serengeti upo mashakani.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa halmashauri ya Loliondo, Methew Siloma alisema msimamo wao bado wanapinga kutengwa eneo hilo kwa kuwa ni la vijiji na wanataka kutafutwa suluhu.
Mbunge Geita, Joseph Kasheku (Msukuma) ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo alieleza kuwa ameona udhaifu uliopo katika utunzwaji wa eneo hilo na kutaka jamii inayozunguka eneo hili ishirikishe ili kutambua umuhimu wa eneo hilo.
Wabunge wengine Mheshimiwa Grace Kiwelu na mheshimiwa Lucy Owenya wa viti maalum mkoa Kilimanjaro wameshauri kutazamwa maslahi mapana ya taifa katika kulinda ikolojia ya Serengeti.
Kwaupande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema dhamira ya serikali ni kuhakikisha ikolojia ya Serengeti inalindwa kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.
Eneo hilo la pori Tengefu la Loliondo lenye kilomita za mraba 4000, limeingia katika mgogoro baada ya wizara ya Maliasilina Utalii, kutangaza uamuzi ya kutaka kulitenga eneo la kilomita 1500 kwa ajili ya uhifadhi na eneo lililobaki kurejeshwa kwa halmashauri ya Ngorongoro.

Mtafiti mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania Dkt. Edward Kohi(wa kwanza kulia) akitoa maelezo ya kitaalamu kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi maliasili na Utalii waliotembelea Pori Tengefu la Loliondo, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

Waziri wa Maliasili na utalii Mhe. Prof Jumanne Maghembe akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati walipotembelea Pori Tengefu la Loliondo

Mfugaji wa jamii ya kimasai Senditwa Maseke akiwaeleza jambo kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi maliasili na Utalii baada ya kukumkuta akichunga ng’ombe ndani ya Pori Tengefu la Loliondo